The House of Favourite Newspapers

Simba yamuwinda kiraka wa Azam FC, Yannick Bangala

Kiraka wa Azam FC, Yannick Bangala

INAELEZWA kuwa Simba ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiraka wa Azam FC, Yannick Bangala ambaye aliibuka hapo akitokea kikosi cha Yanga.

Bangala amekuwa na mwendelezo mzuri ndani ya Azam FC licha ya kuwa alianza msimu kwa mwendo wa kinyonga kwa kuwa hakuwa fiti asilimia mia.

Kiraka huyo ni shuhuda wa timu hiyo ikigotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na inakwenda kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/25.

Inaelezwa kuwa Simba wamewasiliana na wakala wa Bangala ili kumshawishi kiungo huyo raia wa DR Congo kujiunga na timu yao ndani ya dirisha hili kubwa la usajili.

 

Nyota huyo wa zamani wa AS Vita, Far Rabat na Yanga,alisaini mkataba wa miaka miwili na Azam hivyo Simba watatakiwa kukaa mezani na timu yake ili kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki ikiwa wanahitaji kuipata saini yake.
Simba kwa msimu wa 2024/25 itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika na Azam FC ni Ligi ya Mabingwa Afrika.