The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Kuwania Tuzo Za CAF 2024

0

Miamba ya soka ya Tanzania Simba na Yanga, wametajwa kuwania kipengele cha Klabu bora ya mwaka katika tuzo za shirikisho la soka Afrika (CAF), zitakazotolewa Disemba 16 mwaka huu nchini Morroco, wakiwa sambamba na mabingwa wa kihistoria Al Ahly.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Disemba 16 mwaka huu, katika jiji la Marrakech Morroco, Klabu za Simba na Yanga zitachuana na Al Ahly, Mamelodi Sundows, Tp Mazembe, Petro Atletico, Zamalek, RS Berkane, Dream FC na Esperance de Tunis katika kipengele cha Klabu bora ya mwaka.

Yanga na Simba zilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa msimu uliopita, ambapo Klabu ya Yanga ilitolewa na Mabingwa wa Afrika kusini Mamelodi Sundows, wakati wekundu wa msimbazi waking’olewa na Mabingwa Al Ahly.

Kipengele kingine kilichotajwa ni mchezaji bora wa ndani ambapo golikipa wa Mamelodi Sundows Ronwen Williams anachuana na Hussein El Shahati na nyota wengine.

(imeandaliwa na @klaus_kabungu)

Leave A Reply