The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAPANGWA NA WABABE WA SWAZILAND

Klabu ya Simba imepangiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Mbambane Swallows ya Swaziland.

Mechi ya kwanza itafannyika jijini Dar es Salaam kati ya terehe 27-28 Novemba 2018 na ya marudiano itapigwa huko Swaziland 4-5 Disemba 2018.

Mechi hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa Simba msimu huu na pia itakuwa inaanza kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya kuikosa kwa takribani miaka mitano nyuma.

Wakati huo kikosi cha Simba kimeendelea kujifua na mazoezi jijini Dar kwa ajili ya mechi zake zijazo za ligi ikiwa sambamba na maandalizi ya kuelekea mashindano hayo ya kimataifa.

Comments are closed.