The House of Favourite Newspapers

Simba Yapiga Chini Bonge la Kiungo

0

BODI ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, imesitisha mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa Plateau United ya nchini Nigeria, Isah Ndala. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu wakamilishe usajili wa kiungo raia wa Uganda, Taddeo Lwanga.

 

Simba katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 15, mwaka huu, Ndala alikuwepo kwenye mipango yao. Nyota huyo aliisumbua safu ya kiungo ya Simba wakati walipocheza dhidi ya Plateau kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu na kuthibitishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda timu hiyo haitasajili kiungo mwingine mara baada ya kukamilisha usajili wa Lwanga.

 

Kaduguda alisema kuwa wamepanga kusajili wachezaji wawili pekee ambao ni beki wa kati na mshambuliaji namba tisa pekee.

 

“Ilikuwepo mipango ya kumsajili Ndala lakini hivi sasa haipo tena kwani tayari tumemsajili Lwanga anayecheza nafasi hiyo,” alisema Kaduguda.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply