Simba yashusha Wabrazili Watano

SIMBA haitanii aisee! Ni baada ya jana kumsajili Mbrazili mwingine, Gerson Fraga Vieira, 26, kiraka anayecheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji namba 6.

 

Huyo, ni mchezaji wa pili kutoka Brazil kusajiliwa na Simba kwenye msimu huu, ni baada ya hivi karibuni kutangaza kumsajili mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva.

 

Simba hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kusajili wachezaji wapya watano pekee ambao ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman, Silva na Vieira mwenyewe.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, kiraka huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo inayojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiraka huyo amesajiliwa na Simba kwa mujibu wa mapendekezo aliyoyatoa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems katika kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao.

 

Mbrazili huyo jana alitambulishwa katika timu hiyo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zachariah Hans Pope.

 

Silva aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya ya vijana ya U17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson.

 

Pia, aliwahi kucheza timu ya taifa ya vijana ya U20 ya Brazil na alicheza klabu kadhaa za nchini huko ikiwemo ya Grêmio na amejiunga na Simba akitokea ATK FC ya nchini India.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti hili kuwa, Simba imepanga kuwasajili Wabrazil wengine watatu ambao wapo njiani kutambulishwa baada ya kufi kia muafaka mzuri na viongozi wa timu hiyo katika kukiimarisha kikosi chao na kufanya kufi kia Wabrazili watano.


Loading...

Toa comment