The House of Favourite Newspapers

Simba Yasuasua Kupata Bosi Mpya

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi.

UONGOZI wa Klabu ya Simba umefunguka kuwa bado Bodi ya Wakurugenzi pamoja na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo, hazijakutana na kujadili suala la nafasi ya mwenyekiti mpya wa klabu baada ya Swedy Nkwabi kujiuzulu.

 

Simba ilitangaza rasmi Septemba 14, mwaka huu kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi alijiuzulu sababu ikitajwa kuwa ni majukumu yake binafsi.

 

Kutokana na kujiuzulu kwake, Simba inatakiwa kufanya uchaguzi wake ndani ya siku 90 ili kujaza nafasi hiyo ya mwenyekiti mpya wa klabu hiyo.

 

Katibu Dkt Anorld Kashembe amesema kuwa kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha pande hizo mbili zinakutana na kuweza kujadili suala hilo.

 

“Kwa sasa kinachopambaniwa ni muda wa kuhakikisha bodi ya wakurugenzi na kamati ya uchaguzi zinapata muda wa kukutana na kujadiliana suala hilo kuona wanafanya nini ndiyo mambo mengine yaendelee.

 

“Kinachokwamisha kwenda kwa wakati ni uwepo wa wajumbe wote ambao wanatakiwa kukutana kama unavyofahamu kila mmoja ana majukumu yake, wakati mwingine wanapatikana wachache, hivyo kwa sasa watakutana wakati wowote pale watakapokuwa wamekubaliana ni lini na taarifa tutatoa,” alisema Kashembe.

Stori: Martha Mboma, Dar es Salaam

KMC Yapigwa FAINI, ZAWADI MAUYA Apewa ONYO Kali, Mtendaji VPL Azungumza!

Comments are closed.