The House of Favourite Newspapers

ads

Breaking: Simba Yatoa Tamko Kuhusu Kocha wa Makipa “Hakuwa Muajiriwa wa Klabu”

0
Kocha wa makipa Muharami Said Mohammed maarufu ‘Shilton’.

 

Muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa ya Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Said Sultan kukamatwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Klabu hiyo imetoa tamko na kueleza kuwa hakuwa muajiriwa wa klabu hiyo.

 

Taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu ya Simba, imeeleza kuwa Muharami hakuwa mwajiriwa bali aliombwa kuwanoa makipa kwa muda wa mwezi mmoja wakati klabu ikiendelea kutafuta kocha wa magolikipa.

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, haihusiki na tuhuma zinazomkabili kocha huyo na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yoyote inayoweza kuikumba klabu hiyo kutokana na kadhia iliyomkumba kocha huyo.

 

Taarifa ya Muharami pamoja na watuhumiwa wengine 8 kukamatwa, zimetolewa leo na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Leave A Reply