The House of Favourite Newspapers

SIMBA YATOKA SARE NA ASANTE KOTOKO, SIMBA DAY

Kikosi Cha Klabu ya Simba kilichoanza kipindi cha kwanza dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.
Wachezaji wa Timu ya Asante Kotoko kama wanavyoonekana kabla ya mchezo huo.
Emmanuel Okwi akimtoka mchezaji wa Timu ya Asante Kotoko katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Timu ya Simba, Chama Chota akijaribu kumtoka mchezaji wa Asante Kotoko.
Wachezaji wa Timu ya Simba wakijadiliana baada ya kufungwa bao la kwanza dhidi ya Asante Kotoko.

SIMBA leo imecheza na Timu ya Asante Kotoko ya kutoka Ghana ukiwa ni mchezo maalum wa kusherehekea Tamasha la Simba Day lililofanyika katika Uwanja wa Taiafa jijini Dar es Saalaam.

 

Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ambapo  mfungaji bao la simba ni Emmanuel Okwi aliyefunga  dakika ya 76 kipindi cha pili, Adam Salamba akikosa penati dakika ya 83 kipindi cha pili.Kwa upande wa timu ya Asante Kotoko mfungaji wa bao hilo ni  Obeid Owusu dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

 

Simba Day ni mfululizo wa wiki ya Simba ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka na kilele chake kinakuwa tarehe 8, Agosti ambayo ni leo.

 

Siku hii Simba huitumia kwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya siku ambayo inafahamika kama Simba Day.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL


 

Comments are closed.