Kartra

Simba Yatua AS Vita Kumsaka Beki Kitasa

BEKI wa kulia wa AS Vita, Djuma Shabani amekiri kuwa ni kweli alifuatwa na viongozi wa Simba ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

 

Djuma amekuwa katika kiwango bora ndani ya AS Vita ambapo msimu huu katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo amefunga mabao 6 na kutoa pasi tano za mabao.

 

 

Akizungumzia uwezekano wa kutua Simba Djuma amesema: “Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Simba walinitafuta kwa ajili ya mazungumzo ya awali ya usajili lakini siwezi kulizungumzia sana hilo kwa sasa.

 

 

“Hii ni kwa sababu wote kwa sasa tunapambana kuzisaidia timu zetu zifanye vizuri katika michuano ya kimataifa ikizingatiwa tupo kundi moja, ” .

 

 

Ikiwa nyota huyo atamalizana na mabosi wa Simba atakwenda kuongeza nguvu upande wa beki wa kulia na kusaidiana na Shomari Kapombe ambaye ni chaguo namba moja la Didier Gomes.


Toa comment