Simba Yatua Mbeya Kibabe, Mbeya City Wajipange
KIKOSI cha Klabu ya Simba jana kiliwasili rasmi jijini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Mbeya City, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine huku kikitambia rekodi yao kali.
Mchezo huu utakuwa wa kwanza kwa Simba na Mbeya City kukutana msimu huu, ambapo mpaka sasa Simba inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi zao 26 huku Mbeya City wao wakiwa kwenye nafasi ya 15 na pointi zao 12 pekee.
Rekodi zinaibeba Simba kuelekea mchezo huo ambapo, kati ya michezo saba waliyokutana kwenye Uwanja wa Sokoine, wenyeji Mbeya City wameibuka na ushindi kwenye mchezo mmoja pekee huku Simba wao wakifanikiwa kushinda kwe michezo mitano na mchezo mmoja uliosalia ukiisha kwa sare.
Msimu uliopita Simba ilikusanya pointi zote sita dhidi ya Mbeya, ilianza kwa kuipiga ushindi wa mabao 4-0, Novemba 3 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa jijini Dar na kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Juni 24, jijini Mbeya.
Stori: Joel Thomas, Dares Salaam