The House of Favourite Newspapers

Simba Yawafuata FC Platinum na Full Muziki

0

JESHI la wachezaji 24 wa Simba leo Ijumaa Desemba 18, 2020 wamekwea pipa kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Simba imefuzu hatua ya kwanza baada ya kuitoa Plateau United ya nchini Nigeria katika hatua ya awali kwa ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa ugenini.Wachezaji watatu wanatarajiwa kuachwa katika msafara huo ambao ni Larry Bwalya, Charles Ilanfya na kiungo mpya Taddeo Lwanga aliyesajiliwa wiki iliyopita.

 

 

Leave A Reply