The House of Favourite Newspapers

Simba Yawafungia Wanachama Dr. Mohammed na Agnes

0

 

Sekretarieti ya Klabu ya Simba imewafungia kujihusisha na masuala ya klabu Wanachama Mohamed Khamisi Mohamed maarufu Dr. Mohammed na Agnes
M. Daniel maarufu Aggy Simba mpaka pale kamati ya maadili itakapoamua vinginevyo.

Sekretarieti imepoke malalamiko mengi ya kimaadili dhidi ya Wanafamilia hao wa klabu ya Simb ikiwemo kuitisha mikutano kinyume na taratibu na kuchochea migogoro ndani ya Klabu.

Sekretarieti itawafikisha Wanachama hao mbele ya Kamati ya maadili hivi karibuni.

Vamuzi huo umefikiwa kwa Mamlaka ya Sekretarieti iliyonayo chini ya Ibara
ya 31(4)(g) ya katiba ya Simba ya klabu ya 2018 (kama ilivyofanyiwa mareke-bisho 2024), katika kuhakikisha Mahusiano ndani ya Klabu, Wanachama, na Mashabiki hayaathiriwi.

Sekretarieti inawakumbusha wanachama na mashabiki kuheshimu Katiba,
Kanuni, na Miongozo iliyopo ndani ya Klabu.

 

Leave A Reply