Simba:Tutawafunga Yanga kwa Mkapa

MABOSI wa Simba wameweka wazi kuwa wanatambua juu ya mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 11 na wanaamini kwamba watashinda.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Pablo Franco ambaye alichukua mikoba ya Didier Gomes ambaye aliomba kuondoka baada ya timu hiyo kupoteza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneg Galaxy kwa kufungwa mabao 3-1, Uwanja wa Mkapa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba,Salim Abdallah, ‘Try Again’ amesema kuwa kila kitu kuelekea kwenye mchezo huo kipo sawa na wana amini watashinda mchezo huo.

“Desemba 11 tuna mchezo mkubwa na mgumu lakini hatuna hofu kwa kuwa tunawajua tunaamini kwamba tutawapiga na mbinu zao zote tunazijua hivyo kikubwa mashabiki lazima tushirikiane.

“Tunawachezaji wazuri ambao wamesajiliwa na hilo tunajivunia nalo na kwa mechi zetu ambazo tunacheza zote zina umuhimu na kikubwa ni kuona kwamba tunashinda,”.

Simba ni mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi sita za ligi wamekusanya jumla ya pointi 14 wakiwa nafasi ya pili na Yanga wapo nafasi ya kwanza na pointi zao ni 16.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment