SIMIYU: Mwanafunzi Darasa la Pili Atekwa, Auawa!

MWANAFUNZI wa shule ya msingi Lukungu kata ya Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu, Joyce Joseph miaka 8 aliyekuwa akisoma darasa la pili katika shule hiyo ametekwa na watu wasiojulikana na kumuuwa na kisha mwili wake kutelekezwa kichakani.

 

Wakiongea kwa jazba baadhi ya wananchi waliokuwepo katika msiba huo wamesema kwa hivi sasa wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo kwani kwa kipindi kifupi, watoto wadogo wanne na binti wa miaka 21 wameshauawa.

 

Matukio hayo sasa yamewafanya wananchi wa Kata ya Lamadi na wilaya ya Busega kuishi kwa hofu kubwa huku wazazi wakilazimika kuwasindikiza watoto waendapo mashuleni kwa kuhofia watoto wao kutekwa na kuuwawa.

 

Hivi karibuni kuliibuka matukio kadhaa ya utekaji na mauaji ya watoto mkoani Njombe ambapo Serikali ilikwenda kupinga kambi kuhakikisha inatokomeza unyama huo.

CREDIT: ITV

Loading...

Toa comment