Simu ya Kipekee VIVO 23 5G, Kuzinduliwa Kibabe Dar – (Picha +Video)

MAOFISA kutoka VIVO Tanzania leo Februari 25, 2022 wamefika katika mjengo wa Global Group Sinza Mori na kufanya mahojiano na + 255 Global Radion kisha kutambulisha ujio wa simu mpya aina za VIVO 23 5G.
Maofisa hao wa kitengo cha masoko wamesema kuwa zimebaki siku tatu tu kuelekea kilele cha uzinduzi wa toleo lao jipya la V23 5G ambalo litazinduliwa Februari 28, 2022 China Plaza, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Kwa wateja wanaohitaji simu hii wanatakiwa kuweka Pre-oder kwa kulipia shilingi 100,000/- katika ofisi yao na baada ya hapo wanatakiwa kuwepo kwenye wa uzinduzi kwa ajili ya kukabidhiwa simu pamoja na na zawadi mbalimbali siku ya uzinduzi.
Baadhi ya sifa za hiyo ni ukubwa wa kamera ya mbele yenye Megapixel 64 na kamera tatu za nyuma zenye uwezo wa juu zaidi, huku kioo cha simu hiyo kikiwa na ukubwa wa nchi 6.44.

Pia simu hiyo imeboreshwa zaidi kwenye upande wa betri ambapo ina uwezo wa kuchaji betri yake kwa muda mfupi huku ikiwa na ukubwa wa 128 GB na RAM 8.
Aidha hii ni simu pekee yenye uwezo wa kubadilika rangi kila inapokutana na mwanga wa jua.
Mwisho wa kuweka kuweka oda yako ni Februari 27, 2022.

