Simulizi ya JB: Aanza kuachana na uigizaji taratibu
ILIPOISHIA
Msanii wa filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ anaendelea kusimulia historia ya maisha yake. Wiki iliyopita alizungumzia jinsi alivyoamua kuzigawa filamu zake katika Kampuni ya Jerusalem, zile za bajeti ndogo na kubwa na jinsi alivyoanza kuwalipa mishahara wasanii wenzake.
ENDELEA NAYE…. “Swali la kwa nini nisiende kimataifa kama ilivyokuwa kwa marehemu Kanumba na wengine, limekuwa kama kero kubwa kwangu, kila mmoja anatarajia iwe hivyo, kwa nini? Ngoja niseme jambo moja muhimu,” anasema JB na kukaa vyema kitini.
“Haihitaji mtu kucheza sinema na wasanii wa nje kama Nigeria au Ghana ndipo uone kama umefikia kiwango cha juu cha uigizaji, siyo lazima kabisa,” anasema JB kwa msisitizo.
“Mbona hao Wanaigeria na Waghana hawakazani sana kwenda kuigiza nje au kuja huku Tanzania?,” anasema kwa mtindo wa kuhoji.
Hata hivyo, JB anasema kwa sasa anafikiria kuachana na mambo ya kuigiza filamu nyingi zaidi, zaidi ya kujikita katika kutengeneza na kuibua vipaji vipya, lengo likiwa ni kuweka alama kwenye kampuni yake ya Jerusalem, hata ikitokea hayupo, basi kampuni hiyo iendelee kukuza wasanii wengine.
“Kwa hiyo nitakuwa naigiza filamu mbili au tatu tu kwa mwaka mzima, lakini hiyo haimaanishi kuwa sitahusika na filamu, naomba nieleweke kwa hilo,” anasema kisha kukohoa kidogo.
“Nitakuwa nasimama kama muongozaji wa sinema na mtoa ushauri lakini kwa kasi na ladha ileile ambayo watu wameizoea kutoka kwangu,” anasema.
“Ngoja nikueleze jambo moja muhimu pia, unajua kuna watu ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuigiza kuliko mimi? Na kuliko hata marehemu Kanumba lakini tatizo limekuwa ni kwa namna gani wanaweza kutoka na kufikia ndoto za malengo yao,” anasema.
Hapohapo, napata wazo la kumuuliza JB kwa hisia kali kidogo, nataka kujua ni jinsi na namna gani JB amekuwa akiwasaidia watu ambao wana vipaji vya kuigiza lakini hawajui ni wapi pa kuanzia, hususan wale wa mikoani.
“Yeah, ni kweli kabisa nafuatwa na watu wengi sana wakitaka msaada wa kufanikisha ndoto zao za uigizaji, kwa kweli idadi ni kubwa sana na ukiangalia uhalisia kuwa naonekana kuwa mtu mwenye jina kubwa katika tasnia ya uigizaji, ni wengi,” anasema na kuniangalia usoni kidogo na kisha kuendelea.
“Unajua si rahisi kuwasaidia watu wote wenye mahitaji ya kuigiza, sidhani kama inawezekana kabisa kwamba kila mtu anayehitaji kuigiza, nimchukue kwenye kampuni yangu,” anasema.
“Mara nyingi huwa nawapa njia za kufanya ili kufikia malengo yao, kwa wale wa mikoani huwashauri watafute vikundi ambako ndiko kuna mizizi ya uigizaji, huko watajifunza kanuni zote za uigizaji pamoja na nidhamu kama vioo vya jamii,” anasema.
“Pia, kuna watu ambao nimewasaidia sana hadi leo wanaonekana kuwa ni mastaa maarufu, mfano watu kama Shamsa Ford na Wellu Sengo na hata marehemu Adam Kuambiana, wote hawa ni matunda yangu katika sanaa,” anasema JB kwa utulivu.
“Lakini, hadi sasa naendelea kuhakikisha kuwa kuna watu wanarithi mikoba yetu ya uigizaji, huko mitaani kuwa akina JB na Kanumba wengi sana, wakati mwingine huwa nawaunganisha kwa wasanii wengine wenye nafasi na huwachukua, lakini nataka nishauri tena jambo ambalo nimekuwa nikilisisitiza kila mara katika maisha haya ya uigizaji,” anasema mfululizo huku akihema kwa kasi.
“Watu wasipende kuamka asubuhi na kukutana na nafasi za kuigiza kwenye filamu na watu maarufu bila kuanzia ngazi za chini kama vikundi vya maigizo na kwingineko, sanaa hii ina maeneo mapana na yenye mtazamo mkubwa, muigizaji bora na sahihi ni yule anayepitia vikundi,” anasema.
“Wewe angalia wasanii wote waliopitia kwenye vikundi, kwanza hawajashuka viwango vya uigizaji, hakuna kabisa, nani muigizaji wa kike hawa waliochipukia unaweza kumlinganisha na mtu kama Thea, Monalisa, Johari au Koletha, hawa wamepikwa wakapikika vikundini, wataendelea kuwa vinara siku zote,” anasema JB.
“Angalia akina Tino, Swebe, Richie, mtu kama Riyama, na wengine wengi ambao wamepitia vikundi, wameendelea kuwa wasanii wakongwe wasiochuja,” anasema JB huku akichukua glasi yake ya maji.
“Si lazima vikundini tu, pia kuna vyuo vya sanaa, watu waende wakajifunze ili wawe waigizaji bora wa vizazi vijavyo, kuna kile chuo kama cha Kaole kule Bagamoyo, watu waende,” anasema JB.
“Kuna msanii mmoja ngoja nilimzungumzie kwa hisia kabisa, ni mtu ambaye napenda sana kujifunza mambo mengi kutoka kwake, huyu ni Baba Haji (Haji Adam), huyu licha ya ukongwe wote, lakini bado aliamua kuacha mambo yote na kwenda Bagamoyo chuoni kujifua tena. Ukiona ishara hizi kwa mwanaume, jua hakutaki!
JUMAMOSI nyingine msomaji wa safu hii tunakutana na kuweza kupeana darasa la uhusiano. Kwa tuliokuwa pamoja, wiki iliyopita tulijifunza umuhimu wa kumfuatilia mpenzi wako kwa kiasi kinachotakiwa.
Kumpa uhuru uliopitiliza mwenzi wako wakati mwingine kunachochea vishawishi ambavyo pengine vingeweza kuzuilika. Kumfuatilia mtu ni upendo. Mfuatilie ili aone unamjali na aepukane na vishawishi.
Tukirudi katika mada ya leo, wanawake wengi sana wamekuwa wakilia kwa marafiki zao na wakati mwingine kuomba ushauri. Kwamba ameishi na mwanaume kwa kipindi kifupi au kirefu lakini ghafla anaona mabadiliko kwa mwanaume.
Licha ya kuona mabadiliko hayo, wengi wao huwa hawakubaliani na matokeo kwamba, mwanaume hakutaki. Hataki kuamini kwamba mwanaume huyo alikuwa na kitu anachokihitaji na alipokipata anabwaga manyanga.
Hakubaliani na ukweli kwamba huenda mwanaume ameona yeye si sahihi katika uchaguzi wake na kuamua kusonga mbele kutafuta au tayari kampata mwingine. Hapo ndipo penzi linapogeuka maumivu kwa upande wa mwanamke.
Anatumia kila mbinu kuhakikisha hampotezi mwanaume huyo. Anaamini ndiyo chaguo lake, anakuwa mtumwa wa mapenzi bila kujijua. Ameshindwa kabisa kusoma alama za nyakati na kuona anapohangaikia si mahali pake.
Mtoto wa kike anajichosha kwa kujiuliza maswali mengi bila majibu. Anajiuliza amefanya kitu gani kibaya ambacho kimemkera mpenzi wake. Anajiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Anakuwa bize kumfanyia vitu tofautitofauti mpenzi wake ili kuweza kurudisha uhusiano wa kawaida lakini wapi.
Mbaya zaidi, baadhi ya wanaume hao huwa wakiulizwa na wapenzi wao wawaambie wamekosa nini ili pengine wajirekebishe huwa wanakuwa na majibu rahisi tu: “Hujanikosea mbona mimi naona tuko vizuri tu, hakuna tatizo mbona.”
Anasema wako vizuri mdomoni lakini moyoni ana lake jambo. Haoneshi ushirikiano kwa mwenzake, yeye anakuwa kimya tu lakini akiulizwa anasema hakuna tatizo huku akiendelea kutafuta au tayari anakuwa na mwanamke mwingine.