The House of Favourite Newspapers

Simulizi ya Mpoto: mke wangu ananifanya nikwepe skendo

TX4A1433-1200x930Mrisho Mpoto

MPENZI msomaji wa simulizi hii tamu na ya kusisimua ya Mrisho Mpoto, wiki iliyopita tuliishia pale alipotoboa siri ya muziki wake anaoufanya ambapo aliongelea kwa nini amehamua kuwa anatoa wimbo mmoja kwa kila mwaka.

Pia Mrisho aliongelea heshima kubwa aliyojijengea katika muziki wake nje ya Tanzania na kuitwa kwenye majukwaa makubwa kufanya shoo.
Songa nayo mwenyewe sasa…

Mrisho sasa hivi umeingia ubalozi na makampuni mbalimbali nchini? Labda siri na safari ya mafanikio haya ilianzia wapi?
“Labda nieleze siri kubwa ya mtu ama msanii kuwa balozi wa makampuni nchini.

“Hadi sasa nimeshakuwa balozi wa makampuni mengi ambayo ukisema nianze kuyataja hapa nadhani hadi mengine nitayasahau ila kifupi nilishawahi kuwa balozi wa Save the Children, Delight ambayo ilikuwa inasaidia mwanga mashuleni na mengineyo.

“Nimeshakuwa balozi wa mfuko wa pensheni (Pspf) hadi sasa ni mwaka wa tatu huu, kikubwa ili uwe balozi unatakiwa uwe makini na mwenye upeo wa kufikiria, uwe na nguvu ya ushawishi na usiwe na kashfa pia kikubwa uwe na uwezo wa kubeba image yao na kuleta mabadiliko katika kile wanachokifanya.

Kama utaangalia vigezo vyote hivyo ninavyo na ndiyo maana kote huko nimekuwa balozi bila wasiwasi.”

Tuendelee na simulizi yetu Mrisho, tangu umeanza mpaka sasa hujaelezea kama ulishawahi kukumbana na skendo yoyote na nini kilifanyika? (anacheka kidogo)
“Kama nilivyosimulia mwanzoni mwa simulizi hii ya kweli, sijawahi kukutana na skendo ama kuharibiwa na mtu maneno.

Kutokana na maisha niliyokuwa nimejijengea tangu utotoni, nilikuwa mtoto wa mama naweza sema hivyo kama vijana wa siku hizi wanavyosema.

Nilikulia maisha ya kujilinda mwenyewe, maisha ya kumthamini mtu na kuogopa matendo mabaya na hata nilipoingia katika uhusiano na mke wangu (Mariam) naye alikuwa mtu wa dini na kizuri zaidi alikuwa akiimba kaswida sehemu mbalimbali ambapo nami nilikuwa mhudhuriaji.

“Kwa hiyo utaona safari yangu ya kimaisha ilivyokuwa imetawaliwa kwa kiasi kikubwa na imani ya dini pamoja na malezi bora kutoka kwa mama na mke wangu (Mariam), na kitu kikubwa ambacho najivunia nacho mpaka leo hii ni kwa jinsi mama yangu alivyokuwa akihakikisha mtoto wake nakuwa katika mstari sahihi namaanisha kumjua Mungu, kupenda wenzangu sambamba na kuwasaidia kila mmoja na ndiyo kitu ninachoendelea kukifanya kila kukicha.

“Kwa hivi vyote nadhani nimeeleweka ni kwa jinsi gani nipo tofauti na kitu kinachoitwa skendo, kwa jinsi gani nimekwepa skendo za mjini, kwanza hata mtu akurupuke na kusema eti Mrisho kaonekana sehemu fulani na totoz au kafanya kitu kibaya watu watakushangaa kwa sababu kitu kama hicho ni kama ndoto kwangu, hakiwezi kunitokea kabisa.”

Comments are closed.