The House of Favourite Newspapers

Singeli Michano: Sholo Mwamba Aingia Kifalme Dar Live

dar-live-3Shollo Mwamba.dar-live-1Baadhi ya mashabiki wakiserebuka.  Shollo Mwamba baada ya kupandisha jukwaani akiwa amebebwa kifalme.dar-live-1dar-live-4Escide akiwa jukwaani na madensa wake.dar-live-3Dogo Nigga akishambulia jukwaa.dar-live-5Msaga Sumu akifanya yake jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki wake.dar-live-2Shollo Mwamba akiwa jukwaani.efm_8881-001Wasanii wa Singeli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Redio Efm (katikaki) na viongozi wengine.efm_8690Francis Sizza, Mkurugenzi Mkuu wa Redio Efm akitoa semina.

efm_8688-001efm_8701-001…Semina ikiendelea Dar Live.efm_8699…Sehemu ya wahudhuriaji.

MKALI wa Muziki wa Singeli Bongo, Sholo Mwamba usiku wa kuamkia leo ameingia kifalme muda mfupi kabla ya kuanza kupiga bonge la shoo la kihistoria lilikwenda kwa jina la Singeli Michano ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Katika shoo hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Redio cha Efm 93.7 Dar kwa kushirikiana na Dar Live, liliwashuhudia wakali zaidi ya 40 wakipanda jukwaa moja la Dar live na kuamsha mwanzo mwisho.

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na maelfu wa mashabiki wa muziki huo, ilikuwa pia ikirushwa live kupitia kipindi cha Genge kinachorushwa na Redio Efm.

Shoo hiyo ilianza mida ya saa mbili kwa wakali hao kupanda huku burudani ya kipekee kwa madensa ikigeuka kivutio kikubwa kwa mashabiki waliohudhuria.

Miongoni mwa waliokinukisha katika shoo hiyo ni MC Kiduku aliyeamsha shangwe kwa ngoma yake ya Kampa Kampa Tena, Duller Makabila na ngoma yake ya Tatizo Nyota, Majid Migomba, Dogo Niga ambaye naye alikuwa kivutio kikubwa kwa ngoma yake ya Nikuite Nani.

Shoo hiyo ilikuwa na sapraiz pia kwa Malkia wa Sauti, Isha Mashauzi ambapo alipanda jukwaani na kuimba nyimbo yake kisha akapiga freestyle ya singeli jambo lililoibua shangwe upya. Kuonesha kuwa shoo hiyo iliweka historia, mkali wa Msaga sumu aliingia kwa namna yake huku akiwa amevaa suti na kuamsha mashabiki kwa ngoma zake matata kama Matobo, Shemeji Unanitega na nyingine kibao.

Sholo Mwamba ndiye aliyehitimisha gurudumu la burudani hiyo iliyokuwa ikiruka kwa mara ya kwanza live kupitia kipindi hicho ndani ya Dar Live ambapo aliingia na madansa wake matata ambao walikuwa wamevalia nguo za wafungwa.

Kabla ya kuanza kwa shoo nzima hiyo, kulifanyika semina maalum ya uzinduzi rasmi wa Muziki wa Singeli ambapo wageni rasmi walikuwa wawakilishi kutoka Basata, TCRA na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Imeandaliwa na Andrew Carlos, Hilaly Daudi/GPL.

Comments are closed.