The House of Favourite Newspapers

Singida Black Stars Yaendeleza ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba Jiji

0

Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara imeendelea tena Septemba 17, 2024 ambapo katika mchezo wa mapema, Singida Black Stars imeendeleza mwenendo mzuri kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba Jiji Fc na kuendelea kujichimbia zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Wakulima hao wa alizeti wamefikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne za kwanza za Ligi Kuu bara 2024-25. Wamefunga magoli 7 na kuruhusu mabao mawili.

Katika mchezo huo kiungo wa Singida Black Stars, Emmanuel Keyekeh raia wa Ghana amechaguliwa kuwa wa mchezaji bora wa mechi (Man of The match) ikiwa ni tuzo yake ya tatu ya ‘Man of the match’ mpaka sasa msimu huu.

FT: Pamba Jiji 0-1 Singida Black Stars
⚽ Emmanuel Keyekeh 1’

Wakiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Sc, Patrick Aussems Singida Black Stars kwenye mechi nne ushindi mara nne.

Kengold 1-3 Singida Bs
Kagera Sugar 0-1 Singida Bs
Singida Bs 2-1 KMC Fc
Pamba Jiji 0-1 Singida Black Stars

AHMED ALLY: SARE YA BILA BILA INA FAIDA PANDE ZOTE-WAPINZANI WALIKUWA WAZURI

Leave A Reply