The House of Favourite Newspapers

Singida Black Stars Yamtangaza Mtendaji (CEO) Mpya

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kumteua rasmi Omari Kaya kuwa Katibu Mkuu Mtendaji (CEO) wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Jonathan Kassano ambae alikuwa CEO wa Klabu hiyo.

Taarifa ya leo Aprili 12, 2025 iliyotolewa na Uongozi wa klabu ya Singida Black Stars imebainisha kuwa Uteuzi huo umetokana na mchakato wa ndani uliozingatia sifa, uzoefu, na weledi katika masuala ya Uongozi na usimamizi wa shughuli za klabu.

Kaya amewahi kuhudumu kama CEO wa Namungo FC, Katibu mkuu wa Yanga SC na pia hivi karibuni amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Singida Black Stars.