The House of Favourite Newspapers

Singida Black Stars Yatuma Ujumbe Mzito Simba

UONGOZI wa Klabu ya Singida Black Stars umebainisha kuwa utapambana kuwaondoa wapinzani wao Simba katika hatua ya nusu fainali ili kutinga hatua ya fainali ya CRDB Federation Cup.

Singida Black Stars, Aprili 14 2025 ilipata ushindi mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Kaseja kwenye hatua ya robo fainali iliyochezwa Uwanja wa Liti.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 2-0 Kagera Sugar watupiaji wa mabao wakiwa ni Victorien Adebayo dakika ya 11 na Jonathan Sowah dakika ya 66 yanaipa tiketi timu hiyo kukutana na Simba SC iliyowafungashia virago Mbeya City robo fainali.

Ofisa Habari wa Singida Black Stars amebainisha kuwa baada yakushinda mchezo huo wanatambua mshindani wao katika hatua ya nusu fainali atakuwa Simba hilo haliwapo presha wapo tayari kuwakabili.

“Mchezo wetu wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba hatuna hofu nao kwa kuwa kikosi kipo imara na wachezaji wanauzoefu mkubwa ambacho tunahitaji nikiona kwamba tunapata matokeo nakusonga mbele katika hatua ya fainali.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.