The House of Favourite Newspapers

SINGIDA: Polisi Wanamshikilia Mtuhumiwa kwa Kukutwa na Viungo vya Binadamu

0

Jeshi la Polisi mkoani Singida lina mshikilia mkazi moja wa mkoa wa Tabora wilaya ya Igunga wa kijiji cha Itumba kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu na nyara za serikali.

Akiongea na wandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Bwana Magida Bundala aliyekuwa akitokea mkoani Tabora kuja mkoani Singida kuwa salimia ndugu zake ambayo walikuwa wamewekwa maabusu katika kituo cha polisi cha wilaya ya Ikungi.

Kamanda Sedoyeka amesema mbinu waliyo tumia kumkamata mtuhumiwa huyo ni baada ya askari kumtilia mashaka na kuamua kumkagua wakati akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao ni maabusu na kukuta vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi ya simba, pembe ambayo haija julikana na chupa tatu za mafuta ya simba.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida wameliomba jeshi la Polisi kuhakikisha, linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kuweza kubaini mtandao mzima kwa sababu za imani potofu ikiwemo kupata madaraka wana sababisha vifoo vya binadamu ikiwemo wenye ulemavu wa ngonzi Albino.

Katika hatua nyingine kamanda Sedoyeka amesema jeshi la Polisi mkoani Singida lina washikilia watu wanne wakiwemo mwalimu moja wa shule ya sekondari msungua, mwalimu wa shule ya msingi Italala na wakazi wawili wa kijiji cha  msimihi kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili katika daftari la kudu la wapiga kura.

Leave A Reply