SINGIDA UNITED YAMCHUKUA ‘KOCHA WA SIMBA’

KLABU ya Singida United imemwajiri Kocha Mserbia Dragan Popadic kuchukua Mikoba ya Kocha Moroco mwenye majukumu ya kitaifa ya maandalizi ya timu ya U-17.

Kocha Popadic mwenye rekodi kubwa nchini, aliwahi  kuifundisha timu ya Simba, ameungana na miamba ya soka kutoka katikati mwaa Tanzania, Singida United kwa ajili ya kuongeza nguvu hususani kwa kipindi hiki cha kuelekea Sportpesa, FA Cup na Ligi kuu.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United Ndg Festo Sanga amesema, “Popadic atakuwa kocha Mkuu wa timu akisaidiwa na Dusan ambaye pia ni raia wa Serbia.

Ni takribani mechi zaidi ya 10 sasa ambazo Singida United huku ikipata matokeo yasiyoridhisha, hivyo wamiliki wa timu hiyo wameamua kuwapa kazi Waserbia hao ili kurejesha makali ya kikosi hicho kilichofika fainali ya Azam FA Cup msimu uliopita.

Aidha, Sanga amesema, “Makocha walikuwepo na kikosi tayari wameshapewa taaarifa na kukabidhiwa majukumu mengine ndani ya Singida United.”

Loading...

Toa comment