The House of Favourite Newspapers

Siri Binti Kiziwi Kufutuka Jela Yafichuka

0

MODO au video vixen wa Wimbo wa Binti Kiziwi wa msanii Z-Anto, Sandra Khan almaarufu Binti Kiziwi ameshtua wengi baada ya kutoka jela huko Hong Kong nchini China alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka nane kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya.

 

Mshtuko wa Binti Kiziwi umekuja baada ya kutua Bongo akiwa shavu dodo ambapo siri ya kunenepeana kwake gerezani, imevuja.

 

AREJEA BONGO KIMYAKIMYA

Kwa mujibu wa ndugu zake, Binti Kiziwi alirejea Bongo kimyakimya, Desemba, mwaka jana baada ya kumaliza kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’.

Mrembo huyo ambaye alifungwa Hong Kong, China mwaka 2012 kwa kosa hilo, alimaliza kifungo chake mwishoni mwa mwaka jana, baada ya hapo alirudishwa nchini Tanzania.

 

Hivi karibuni, Z-Anto ambaye ndiye aliyemtambulisha Binti Kiziwi kwenye tasnia ya sanaa baada ya kumuoa 2007, alimtembelea anakoishi jijini Dar na kuzungumza naye mawili-matatu juu ya maisha yake mapya baada ya kurejea uraiani akiwa amenenepa ile mbaya ukilinganisha na kipindi kile alipopata msala huo.

 

SIRI YA KUNENEPEANA

Kwa mujibu wa barua ya video vixen mwenzake ambaye naye anatumikia kifungo kama cha Binti Kiziwi, Jacqueline Patrick aliyoituma kwa mwandishi wetu siku za nyuma, ilibeba siri za maisha yao gerezani.

Barua hiyo ilieleza kuwa, wakiwa gerezani nchini humo, maisha ni bomba mno na wakati mwingine kuyaona ni mazuri kuliko ya uraiani kwa baadhi ya nchi duniani (lakini siyo Tanzania).

 

MAISHA BOMBA GEREZANI

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Jack Patrick, maisha ndani ya magereza ya Hong Kong ni bomba kwani mtu anakula vizuri na anafanya kazi mbalimbali za kuwaingizia vipato kiasi cha kutuma nyumbani kwa wazazi wao huku Bongo.

 

Barua hiyo ilieleza kuwa, wafungwa kama wao wa muda mrefu wana uwezo wa kufanya kazi mbalimbali na kujiingizia kipato na wanalipwa mishahara wakati wapo kifungoni.

 

MATIBABU BURE

Si hilo tu, bali wanapata bure matibabu ya magonjwa yote, ikiwamo upatikanaji wa dawa zote wanapoumwa.

 

PADRI AUNGA MKONO

Hivi karibuni Padri wa Kanisa Katoliki na mkazi wa Guangzhou nchini China, Padri John Wootherspon alifika nchini Tanzania kwa ajili ya kueneza habari ya vita ya biashara ya madawa ya kulevya isienee barani Afrika.

 

Katika maelezo yake, Padri Wootherspon aliunga mkono maelezo ya Jack Patrick kuwa, maisha ya magerezani huko Hong Kong yana unafuu huo.

Padri Wootherspon alisema anatamani kuwe na mbadilishano wa wafungwa kwani asilimia 90 ya wafungwa wa Kitanzania walio magerezani nchini humo, hawataki kurejea makwao kwani wanayaona maisha ya huko ni bomba.

 

Padri John alisema, wafungwa wenye uwezo wa kufanya kazi kama kushona, kuunganisha vitabu, kudarizi, seremala; wanalipwa kati ya shilingi 115,000 na shilingi 185,000 kwa mwezi.

Padri huyo alisema pia wanapata bure matibabu ya magonjwa yote, ikiwamo upatikanaji wa dawa zote za saratani na Ukimwi.

 

“Wafungwa hao hupata nguo mpya kila mwezi na viatu, pamoja na kibali cha kusomea kozi mbalimbali, kuanzia cheti, diploma na shahada ya uzamili,” alisema padri huyo.

 

WANACHAGUA WALE NINI

Kuhusu chakula, Padri Wootherspon alisema wafungwa wanaweza kuchagua wale nini wanachotaka.

“Wengi wanaona nafuu kufungwa Hong Kong kwa kuwa wanaweza kufanya kazi na kupeleka fedha kwa familia zao Tanzania,” alisema padri huyo.

 

HALI IKOJE?

Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Nchini imeanza kuwafuatilia wafanyabiashara wanaowatuma vijana wa Kitanzania kusafirisha madawa ya kulevya nchi za nje baada ya kupata majina kutoka kwa padri huyo.

 

Naibu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, James Kaji alimwambia mwandishi wetu kuwa tayari wamepokea majina ya watu hao kutoka kwa padri huyo. Kamishna alisema hivi karibuni mamlaka hiyo ilikutana na padri huyo ambaye alitoa orodha ya watuhumiwa kama walivyomueleza wafungwa huko China ambao wametokea Tanzania.

 

Kamishna Kija alisema kuwa, watu hao waliotajwa na wafungwa hao, wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na kwamba wameanza kuyafanyia kazi majina yao.

Kamishna huyo alithibitisha mamlaka hiyo kupokea majina ya baadhi ya watu maarufu na wafungwa 130 walio katika magereza ya Hong Kong na China.

 

Akifafanua zaidi kuhusu wafanyabiashara hao, Kamishna Kaji alisema wengine wanamiliki maduka makubwa yakiwemo ya ujenzi, supermarket, maduka ya nguo na uuzaji wa magari katika yadi mbalimbali jijini Dar.

 

Katika orodha ya wafanyabiashara hao, Kamishna Kaji alisema; “Tumeyapokea na taratibu za kiuchunguzi zinaendelea, ili kujua njia wanazotumia kuwatumia hao watu, nia yetu ni kung’oa kabisa mizizi ya tatizo.

 

“Kuna majina nikikuonesha hutaamini ni ‘mabig fish’ (watu wakubwa), wapo mstari wa mbele kulipa kodi na kuisaidia jamii, lakini nyuma ya pazia wanaendesha biashara haramu kwa kutumia watu,” alisema kamishna huyo.

 

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya raia wa kigeni wanakuja nchini na kuwarubuni vijana wadogo kwa kutoa mafunzo na kuwaingiza katika mtandao huo wa dawa za kulevya ikiwemo biashara haramu ya madanguro.

 

Kamishna Kaji alisema kitengo chake kipo mstari wa mbele katika kupambana dhidi ya dawa za kulevya kama vile cocaine, heroine na aina nyingine za dawa ya kulevya.

 

Alisema hapa nchini wamedhibiti utumiaji na uingizaji wa dawa hizo kwa asilimia 98 na kwamba sasa wauzaji wanatumia nchi jirani ya Msumbiji na Afrika Kusini kama uchochoro wa kupitisha dawa hizo.

 

“Kuna Watanzania watatu ambao wamekamatwa mwezi huu wa Januari huko Hong Kong, Watanzania hao walitokea Ethiopia na hawakupitia airport zetu,” alibainisha.

STORI: Imelda Mtema, Risasi

Leave A Reply