The House of Favourite Newspapers

Siri imefichuka… Sarah wa Harmo Kusepa na Range za Kajala, Atinga Mahakamani

0
Mwanamitindo wa kimataifa wa nchini Italia, Sarah Michelotti.

Sarah Michelotti; ni mwanamitindo wa kimataifa wa nchini Italia ambaye alidumu kwenye uhusiano wa kimapenzi na kindoa kwa miaka minne na msanii Harmonize au Konde Boy kabla ya kuachana mwaka 2020 na sasa ametinga mahakamani kudai talaka na mgawanyo wa mali walizochuma pamoja, IJUMAA lina mchongo wote wa sakata hilo.

 

RANGE ROVER ZA KAJALA ZATAJWA

Septemba 27, 2022, Sarah na jopo lake la wanasheria na wanafamilia walifika katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua madai ya talaka na mgawanyo wa mali huku yale magari ya kifahari mawili aina ya Range Rover Evoque ambayo Harmonize amemnunulia mchumba’ke wa sasa, Kajala Masanja zikitajwa.

 

Sarah ambaye alitengana na Harmonize takriban miaka mitatu iliyopita, aliwasili nchini Tanzania mapema mwezi Septemba ambapo aliweka kambi visiwani Zanzibar.

 

Sarah Michelotti akiwa na Harmonize enzi hizo.

Katika kipindi cha siku kadhaa ambazo zimepita, Sarah alikuwa akifurahia maisha katika kisiwa hicho cha marashi ya karafuu na kufichua kuwa yuko katika Kijiji cha Kiwengwa visiwani Zanzibar.

 

“Najihisi nyumbani…Zanzibari,” Sarah alisema wakati akila bata visiwani humo wiki iliyopita.

 

MARAFIKI WAMPA MCHONGO WA KAJALA

Watu wake wa karibu wameliambia IJUMAA kuwa, Sarah amekuwa akitumia ziara yake ya Tanzania kurudisha kumbukumbu za kipindi ambacho aliishi na Harmonize na kukutana na baadhi ya marafiki zake ambao aliwapata wakati huo na ndiyo wamekuwa wakimpa mchongo wote wa jinsi Kajala anavyowapiga bakora kwa mali alizoshiriki kuzitafuta.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda, Sarah alikuwa ameandamana na kundi kubwa la wanasheria na anakusudia kuvichukua vyote alivyompa Harmonize.

Harmonize au Konde Boy akiwana mpenzi wake Kajala.

 

MALI ANAZOZIDAI SARAH

Watu wa karibu wa Sarah wanasema kuwa, baadhi ya mali ambazo mwanamitindo huyo amezilenga ni pamoja na asilimia ya uanzishwaji wa Lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize, nyumba na magari ambayo aliyaacha wakati anasepa kutoka kwenye himaya ya Harmonize.

 

Inasemekana kwa sasa, Harmonize alishabadilisha magari hayo na kumiliki mengine yakiwemo hayo ya Kajala aina ya Range ambayo yanaweza kuchukuliwa kufidia yale aliyomuachia Sarah.

 

Mwaka jana, Harmonize alitunga wimbo uliokwenda kwa jina la Sorry kwa ajili ya kumuomba msamaha Sarah akieleza namna alivyomuokota na kumsaidia katika maisha yake.

 

Kwa mujibu wa Harmonize, ndoa yao ilianza kusambaratika wakati Sarah alipokuwa amesafiri kwenda kwao nchini Italia na baada ya kuwa mpweke kwa muda ndipo akapata majaribu ya kutembea na mwanamama Shanteel aliyemzalia mtoto wa kike aitwaye Zuuh Konde.

 

“Mimi nilikuwa Tanzania na kama unavyojua umbali wa mapenzi unavyokuwa, nikaishia kutembea na mwanamke ambaye ni Mama Zuuh sasa hivi.

 

“Kwa mipango ya mwenyezi Mungu nikamfanya mjamzito. Akaniambia na kuniuliza ikiwa niko tayari au atoe. Kwa kuwa mimi ni Muislam, kutoa mimba ni kushiriki dhambi. Sikuwa tayari kwa hayo. Niliamua ni njia ambayo Mwenyezi Mungu aliamua kunipitisha,” alisema Harmonize.

 

Harmonize alisema kuwa, Sarah aliumia mno moyoni baada ya kupata habari kwamba alikuwa amecheza karata nje na kupachika mwanadada mwingine ujauzito.

 

Harmonize alieleza kuwa, alijaribu mno kumshawishi Sarah amsamehe ili warejeshe ndoa yao, lakini juhudi zake zote ziliambulia patupu.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar | Gazeti la Ijumaa

NAY KASHINDIKANA, AWAVULISHA MASHATI MASHABIKI AKIPAFOMU, FIESTA MWANZA..

Leave A Reply