The House of Favourite Newspapers

Siri Mondi kumtosa Tanasha yafichuka!

0

WIKIENDI iliyopita gumzo kubwa lilikuwa ni shoo ya uzinduzi wa albam fupi ya muziki (EP) ya mrembo Tanasha Donna Oketch iliyofanyika Nairobi nchini Kenya, kilichojadiliwa zaidi ni kitendo cha mzazi mwenzake, mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ kumtosa, IJUMAA WIKIENDA limenasa siri iliyojificha nyuma ya pazia.

 

Awali, shoo hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Sarit Centre Expo uliopo Nairobi nchini Kenya, ilinadiwa kwa mbwembwe kama zote ikiaminika kuwa Mondi atakuwa ndani ya nyumba.

 

MONDI ATIMKA GHAFLA

Tofauti na matarajio ya wengi, Mondi aliikacha shoo hiyo baada ya kufika Nairobi na ghafla akarejea Bongo:

 

“Kutokana na tatizo la ghafla lililotokea nyumbani, imenibidi niruke Dar es Salaam mara moja kwa ajili ya kulisolve…hivyo naweza kufika nimechelewa au pengine kutofanikiwa kuhudhuria hafla ya uzinduzi maalum ya EP ya mpenzi wangu mjini Nairobi usiku wa leo. Niwakumbushe tu kuwa, event hiyo itakuwa inaruka live kupitia @wasafitv… mlio majumbani msikose kutazama,” aliandika Mondi kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

 

WANANZENGO WAJIONGEZA

Licha ya Mondi kuweka ufafanuzi huo, wananzengo walikwenda mbali zaidi kwa kusema tayari kuna tatizo kati ya wawili hao, hivyo Tanasha ajiandae kisaikolojia.

 

“Haya ndiyo yaleyale yaliyomtokea Zari (mzazi mwenza wa Mondi), Tanasha aanze kujiandaa kisaikolojia maana haiwezekani shoo kubwa kama hii ya mpenzi wake asitokee, halafu hiyo dharura yenyewe aliyoipata hajaitaja,” alisema mdau mmoja kwenye ukurasa wa Instagram.

 

UBUYU MWINGINE

Baadhi ya wambeya wengine waliibuka huko Instagram na ubuyu uliodai kuwa, Mondi alirudi Bongo kwa sababu mama yake alipata shambulio la moyo (heart attack) jambo ambalo IJUMAA WIKIENDA lilibaini halikuwa na ukweli.

“Nasikia mama yake sijui alipata shambulio la moyo ndiyo maana akalazimika kurejea Dar haraka,” aliandika mdau mwingine kwenye Instagram.

WENGINE WAZUSHA AJALI

Kama hiyo haitoshi, kuna wengine walijiongeza kuwa Mondi alilazimika kurejea Bongo ghafla kutokana na mtoto wake na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto, Dyllan kupata ajali.

Hilo nalo lilifuatiliwa kwa kina na IJUMAA WIKIENDA na kubainika kwamba pia hapakuwa na ukweli wowote.

 

SIRI YAFICHUKA

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA liliingia mzigoni kusaka undani wa tukio hilo ndipo lilipokutana na chanzo makini kilichopo ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB) kilichong’amua siri iliyokuwa nyuma ya pazia.

 

“Iko hivi; pale ni ishu ya kibiashara, Mondi alijua kabisa kwamba kama angepafomu pale kwenye ile event ya Tanasha, concentration (umakini) wa mashabiki usingekuwa kwenye uzinduzi wa EP ya mpenzi wake.

 

“Ndiyo maana akahakikisha tu ameitangaza event vya kutosha, lakini yeye hakutokea pamoja na Mbosso. Wangeimba hawa, hata baada ya shoo gumzo lisingekuwa kwa Tanasha badala yake wangemjadili Mbosso na Mondi na kuchukua attention yote,” kilisema chanzo hicho.

 

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, lengo la Mondi lilikuwa ni kutaka kuona mapokeo ya Tanasha na kuanza kumuamini katika shoo zake nyingine anazoweza kuziandaa akiwa mwenyewe bila kutegemea nguvu ya Wasafi.

 

“Ni mpango tu ndiyo maana unaona hata Mbosso alikwenda Kenya, lakini akarudi ghafla, angethubutu tu kubaki hata Mbosso pekee, upepo ungekuwa kwake halafu Tanasha asingeweza kujipima.

“Mpango umefanikiwa na umeona Tanasha amefanya uzinduzi mzuri, anazungumzwa yeye na nyimbo zake nzuri,” kilisema chanzo hicho.

 

MONDI

Gazeti hili lilimtafuta Mondi, lakini simu yake haikuwa hewani. Hata hivyo alipotumiwa chatting kwenye WhatsApp zilionesha amezisoma.

BABU TALE

Mbali na Mondi, pia gazeti hili lilimtafuta mmoja wa mameneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ambaye alisema anaifahamu dharura aliyoipata Mondi, lakini ni jambo binafsi ambalo anapaswa kulizungumzia yeye mwenyewe.

 

MAMA DANGOTE

Kwa upande wake, Mama Dangote alipotafuta na gazeti hili alisema yuko poa, lakini alipoulizwa juu ya Mondi kumtosa Tanasha alikata simu.

 

MBOSSO

Naye Mbosso alipotafutwa alisikiliza maelezo vizuri juu ya kumtosa Tanasha ambaye amefanya naye Wimbo wa La Vie alidai anashuti video hivyo atamtafuta mwandishi baadaye, jambo ambalo hakulitekeleza.

TANASHA KWENYE MUZIKI

Tanasha anaonekana kuja vizuri kwenye ulimwengu wa muziki na kupewa sapoti kubwa na Mondi. Awali mwishoni mwa mwaka jana, alianza kuachia wimbo wake wa Radio aliomshirikisha Barak Jacuzzi, lakini kubwa zaidi ni tukio hilo la uzinduzi wa EP yake iliyokwenda kwa jina la Donnatella.

 

Mbali na EP hiyo, wimbo mwingine uliomuweka juu Tanasha ni ule wa La Vie aliomshirikisha Mbosso ambao ameuachia wiki mbili na ushee zilizopita ambayo hadi jana ulikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 1.9 kwenye Mtandao wa YouTube.

STORI: WAANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply