Siri Vanessa, Jux kuachana!

DAR ES SALAAM: “Mimi na Jux (Juma Khalid) tuliachana zaidi ya miezi tisa iliyopita!” Hayo ni maneno ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ alipotoa siri ya kuachana na mpenzi wake, Jux ambaye kwa sasa ana mpenzi mkali, mwenye asili ya Asia.

 

Stori za Vanessa na Jux kuachana zilisambaa mno mwezi Mei, mwaka huu baada ya mdogo wa Vanessa, Mimi Mars kutoboa siri hiyo.

Baada ya kimya kirefu, hatimaye V-Money ameweka wazi kuwa, ukweli ni kwamba aliachana rasmi na Jux, mwaka jana.

 

Vanessa ametumia Insta Story kueleza kwa nini yeye na Jux hawakuweka wazi kwamba wameachana.

Amesema kuwa, walifanya ishu hiyo kuwa siri kwa muda kwa sababu ya biashara ambazo wanafanya pamoja.

 

“Juma na mimi tumeachana, tuna miezi zaidi ya tisa.

“Tumeachana for a long long long long time. Tumeachana in a way tulikuwa tunajua kwamba tukifanya public ita-affect watu wengi, isitoshe sisi tuna vitu vingi ambavyo tunafanya kwa pamoja kama biashara, tuna vitu vingi ambavyo tulikuwa tunamiliki pamoja in terms of like joint interests.

 

“Kuna vitu ambavyo tulikuwa tumepanga kufanya kwa pamoja and that was the reason why hatukupaswa kutangaza kuachana kwetu mapema,” alisema Vanessa.

Pia Vanessa alimzungumzia mpenzi mpya wa Jux, mwenye asili ya Asia ambapo ameeleza kuwa aligundua pia kuwa Jux alishasepa zake baada ya kumuona akiposti picha za mpenzi wake huyo mpya kwenye mitandao ya kijamii.

 

Vanessa amesema anaamini watu wataacha kumlaumu juu ya kwa nini ameachana na Jux.

Alieleza kuwa, wote wawili walikubaliana kusitisha uhusiano wao huo wa kimapenzi na kubaki kuwa marafiki wazuri.

 

Vanessa alikwenda mbele zaidi na kufunguka kuhusu tetesi za hivi karibuni kuwa anatoka kimapenzi na mchumba wa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Francis Siza a.k.a Majizzo.

Vanessa alisema ishu hiyo ni uongo mtupu na kwamba Majizzo ni kama kaka yake na mfanyabiashara ambaye anamheshimu mno.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Loading...

Toa comment