IRENE PAUL NA BIFU LA ZAMARADI Vs MOBETO
STAA wa filamu Bongo, Irene Paul ameibuka na kutaja sababu za kutoingilia bifu la shoga yake kipenzi, Zamaradi Mketema na Hamisa Mobeto kuwa ni uoga.
Akichonga na Za Motomoto News, Irene alisema Zamaradi alipoingia kwenye ugomvi na Mobeto hivi karibuni kisa kikiwa mshono wa nguo aliyovaa kwenye arobaini ya mwanaye, yeye aliamua kujiweka pembeni kwa sababu aliogopa kuchukuliwa hatua za kisheria kwani serikali kwa sasa haitaki mchezo.
“Si unajua tena siku hizi sheria za mtandao, unaweza kujifanya kimbelembele yakakukuta mazito kwa hiyo niliona nikae pembeni licha ya kwamba Zamaradi ni rafiki yangu sana kwa sababu nilifahamu pia wawili hao wangeweza kumalizana bila tatizo lolote,” alisema Irene.
Stori: Boniphace Ngumije, Dar
Comments are closed.