The House of Favourite Newspapers

Siri ya Mafuriko ya Lowassa, Magufuli yafichuka

0

MagufuliiMgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli akinadi akiomba ridhaa kwa wananchi.

Gabriel Ng’osha na Gladness Malya

NDIYO maana! Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki Maalim Hassan Yahya amepasua jipu kuwa wagombea wawili wa urais katika uchaguzi wa mwaka huu, John Magufuli na Edward Lowassa wanabebwa na nyota zao.

pic+lowassaMgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Ngoyai Lowassa akinadi akiomba ridhaa kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wetu hivi karibuni, alisema kinajimu, herufi M inayosimama badala ya Magufuli, nyota yake ni ya samaki ambayo asili yake ni maji wakati herufi L kwa maana ya Lowassa, nyota yake ni mshale, ambayo kiasili ni moto na ndiyo maana kuna mvutano mkubwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Maji yana nguvu kubwa sana ya kuweza kuuzima moto kama yakimwagikia vizuri huo moto, lakini pia moto nao unaweza kuyafanya maji yakachemka mpaka yakakauka na kuunguza sufuria, hivyo duru ya siasa za mwaka huu chochote kinaweza kutokea,’’alisema Maalimu, mtoto wa mnajimu mashuhuri wa zamani, Sheikh Yahya Hussein.

Hata hivyo, Hassan ameitaka serikali na vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama kuwa makini katika uchaguzi wa mwaka huu kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoanza kujitokeza nchini.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply