The House of Favourite Newspapers

SIRI YA UKIMYA WA KIDOA NI HII

 

 

Image result for Asha Salum ‘Kidoa’,
Asha Salum ‘Kidoa’

WAFUATILIAJI wa maisha ya mastaa watakubaliana na ukweli kwamba, msanii aliyewahi kutingisha kwa vituko, mapicha ya nusu utupu na figa yake ya kufungashia, Asha Salum ‘Kidoa’, amekuwa kimya sana na sasa siri ya ukimya huo imefickuka.

Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, staa huyo anayeshilikia taji la Ijumaa Sexiest Girl 2015 alisema kuwa, vurugu alizokuwa akifanya kipindi cha nyuma kwenye mitandao ya kijamii alidhani zingeweza kumfikisha mbali, lakini haikuwa hivyo, ndiyo maana ameona atulie, afanye mambo yake kimyakimya.

“Nimekuwa kimya sana kwa sababu nimegundua nikiwa hivyo naweza kufanya vitu vingi vya kuniingizia pesa tofauti na huko nyuma. Na ukimya wangu huu napata madili mengi tu, nimegundua kujichetua kwangu kunaweza kuniweka mbali na kazi za pesa. Ndiyo maana niko kimya. Ila nipo, nafanya kazi zangu kama kawaida,” alisema Kidoa.

 

STORI: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.