The House of Favourite Newspapers

Siri Yafichuka Nandy Kufunga Ndoa ya Chap kwa Haraka ‘Zimamoto’ na Billnass

0
Nandy au The African Princes

 

Nandy au The African Princes na Billnass au Nenga; ni wapenzi mastaa wakubwa wa muziki nchini Tanzania ambao wikiendi hii (kesho) wanatarajiwa kufunga ndoa ya chap kwa haraka; ya zimamoto.

 

Kwa mujibu wa familia ya Nandy au Nandera siku ile ya kuvishwa pete ya uchumba mapema Februari, mwaka huu, ndoa hiyo ilipangwa kufungwa haraka ifikapo Juni 25, mwaka huu; yaani kesho.

 

Gazeti la IJUMAA lina nakala ya kadi ya mchango ambayo inasomeka; “Familia ya Bwana Lyimo wa Dar es Salaam ikishirikiana na Kamati ya maandalizi ya harusi kukujulisha kwamba kijana wao mpendwa William Nicolaus Lyimo (Bilnass) anayetarajia kufunga ndoa na Faustina Charles Mfinanga (Nandy) tarehe 25/06/2022 jijini Dar es Salaam kuwa kama ndugu, jamaa na rafiki unaombwa mchango…”

Nandy akiwa na mpenzi wake Billnass au Nenga.

 

Hata hivyo, siri nzito imefichuka kwamba, ndoa hiyo ilikuwa iahirishwe na isifanyike wikiendi hii, lakini imebidi ifanyike haraka kwa sababu tayari uhusiano wa Nandy na Nenga umejibu.

 

Watu wa karibu na Nandy wamevujisha video ikimuonesha malikia huyo wa muziki Afrika Mashariki akiwa na mimba kubwa tu ambayo familia yake inasema siyo sawa na ni aibu kama atajifungua kabla ya kufunga ndoa.

 

Vyanzo vya uhakika vinasema kwamba, kwa sasa Nandy hawezi hata kuchukua pesa za shoo au kufanya projekti yoyote ya kimuziki hasa inayohusisha nguvu kubwa ya kimwili kwani tumbo limekuwa kubwa mno na si ajabu akajifungua muda wowote kuanzia sasa.

 

Mara ya mwisho Nandy kuonekana hadharani ni siku ile alipokwenda kwenye dili la ubalozi, lakini alipoulizwa mbona kitumbo kimekuwa kikubwa alikataa katakata kuwa hana mimba.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Leave A Reply