Siri Zafichuka Kuvunjika Ndoa ya Dida, Kumbilamoto Kuvunjika

 

ILICHUKUA siku 150 tu kabla ya ndoa ya Mtangazaji wa Wasafi FM, Khadija Isihaka Shaibu almaarufu Dida kudaiwa kuvunijika; ikiwa ni ndoa rasmi ya nne katika maisha yake, IJUMAA lina ripoti ya siri nzito.

Ripoti ya Gazeti la IJUMAA imejikita kwenye rekodi aliyoweka Dida mwenye umri wa miaka 39 na ni nini hasa kilijiri kwenye ndoa zake nyingine zilizopita.

MADAI YA KUVUNJIKA NDOA YA 4

Mapema mwezi Novemba, 2021 ndipo yalipoanza kusikika madai mazito juu ya kuvunjika kwa ndoa ya nne na ya kifahari zaidi ya Dida aliyofunga Mwezi Juni, 2021 na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto.

Madai ya kuvunjika kwa ndoa ya Dida na Meya yalishika kasi baada ya mwanamama huyo kuacha kujiita Mama Mheshimiwa na baadaye Mama Meya, lakini ghafla majina hayo yakawa hasikiki tena.

AFIKIA REKODI YA ESMA

Kupitia Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM anachokiendesha Dida, Juma Lokole na Idris Kitaa, watu wakatega masikio kusikia kama atasema lolote juu madai mazito ya kuvunjika kwa ndoa hiyo ikielezwa kwamba, ameifikia rekodi ya dada wa msanii Diamond Platnumz, Esma Platnumz ambaye naye ameolewa mara nne na ndoa zote hizo kuvunjika.

NDOA YA 5 SOON

Ilidaiwa kwamba, baada ya ndoa hiyo kuota mbawa, Dida alianza kujigamba kwamba yupo mbioni kuitafuta ndoa ya tano ‘soon’ ndani ya mwaka 2022 ambapo kama hilo litatokea, basi atakuwa ameifikia rekodi inayoshikiliwa na mwigizaji Wastara ya kuolewa mara tano.

Kwa mujibu wa watu wa karibu, wakati Dida anafunga ndoa na Meya alikuwa ameachana na mtu mwingine ambaye alikuwa naye kwenye uhusiano, lakini mapenzi yao yalikufa baada ya mwanamama huyo kuolewa.

Hata hivyo, vyanzo vya ndani kabisa vidai kwamba, kwa sasa ameamua kurudisha majeshi kwa mpenzi wake huyo wa awali ambaye ni kijana; damu changa.

IJUMAA NA DIDA

Katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA juu ya kuvunijika kwa ndoa yake na Meya, mambo yalikuwa hivi kupitia kuchati kwa njia ya SMS;

IJUMAA: Mambo vipi Dida?

DIDA: Poa.

IJUMAA: Mimi ni Mwandishi wa Gazeti la IJUMAA, kuna jambo zito ningependa kupata undani wake kutoka kwako…

DIDA: Jambo lipi?

IJUMAA: Kuna habari nzito hapa kwamba ndoa yako na mheshimiwa Meya imevunjika, ukweli ukoje?

DIDA: Muulize aliyekupa habari…

IJUMAA: Sawa, lakini ni busara ukaniambia tu ukweli ili na mimi nijue kinachoendelea…

DIDA: Muwe na uhakika kwanza ndugu yangu, mimi siyajui ndiyo nasikia kwako.

IJUMAA: Sawa, nimekuelewa…

DIDA: Mpigie mheshimiwa umuulize vizuri.

Gazeti la IJUMAA lilifanya jitihada za kumpata Meya bila mafanikio kwani simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili naye asikike upande wake.

JUMA LOKOLE APASUA JIPU

Mmoja wa watu wa karibu wa Dida ni Juma Lokole ambaye pia ni mtangazaji mwenzake ambaye anakiri ndoa hiyo kuvunjika huku akidai Dida ndiye ameacha siyo ameachwa.

“Usiseme Dida ameachwa, hapana, Dida ndiye ameacha na anachodai ni talaka, sema yule bwana anasitasita…” Anasema Juma Lokole kwa kujiamoni na sauti yake tunayo.

Wakati baadhi ya wanawake wakiamini kuwa, Dida ana bahati ya kuolewa ndiyo maana amefikisha ndoa nyingi na anaendelea, ngoja tukukumbushe ndoa zake nyingine zilizovunjika;

DIDA NA MCHOPS

Awali kabisa akiwa chini ya umri wa miaka 20, Dida aliolewa kwa ndoa ya kifahari na mfanyabishara maarufu jijini Dar aliyeitwa Mohammed Mchopanga almaarufu Mchops.

Wawili hao walipendana na kapo yao ikawa maarufu kiasi cha Dida kupewa jina la Dida wa Mchops ambalo hadi leo kuna watu wanamuita hivyo.

Katika ndoa yao, Dida na Mchops walijaaliwa kupata mtoto wa kike mkubwa tu kwa sasa aitwaye Samira kabla ya kuachana kwa kile kilichodaiwa ni kushindwana.

DIDA NA G

Baada ya hapo, mwaka 2011, Dida alifunga ndoa ya pili na mfanyabiashara Gervas Mbwiga almaarufu G na ndipo likazaliwa lile jina la Dida wa G.

Ndoa hiyo ilidumu kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuvunjika mwisho mwa mwaka 2012.

Awali, Dida aliliambia gazeti hili la IJUMAA kuwa, ndoa hiyo ilikuwa ni ya mkataba wa mwaka mmoja, lakini uchunguzi ukaonesha ilivunjika kutokana na tofauti za kidini kati ya wawili hao; Dida ni Muislam huku G akiwa ni Mkristo.

DIDA NA EZDEN

Kutoka kwa G, Dida akatua moyo wake kwa Jumanne Ezden ambaye wakati huo alikuwa Mtangazaji wa Tevisheni ya TV1.

Katika kuachana kwao, kila mmoja alitoa sababu zake huku Dida akidai kupokea vipigo kutoka kwa jamaa huyo ambaye kwa upande wake alidai kujifunza mengi kutoka kwa mwanamama huyo.

STORI; WAANDISHI WETU, DAR

4228
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment