The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Sirro Afafanua Utata wa Kifo cha Denti UDSM Aliyedaiwa Kuuawa na Polisi

0
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, akizungumza na wanahabari leo kuhusiana na mbinu wanazotumia wezi wa vyombo vya moto.

DAR ES SALAAM: KAMISHNA wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro,  amesema jeshi la polisi haliwezi kuua raia asiye na hatia.

Sirro aliyasema hayo leo kwa wanahabari alipozungumzia mauaji ya kijana mmoja kwenye mashine ya kutolea pesa (ATM) ya CRDB Bank eneo la  Kurasini jijini Dar es Salaam  ambapo baadhi ya ndugu wa marehemu wanadai hakuwa jambazi kama polisi wanavyodai.

“Naomba niwaeleze watu wa mitandao ya kijamii inayosema kuwa polisi wameua kijana ambaye ni mtumishi wa Mungu na mwanachuo. Ukweli ni kwamba ndugu wanaweza kuona kijana wao anatoka nyumbani kwenda shuleni, kumbe ana mambo yake.

Kamanda Sirro akionyesha bangi na vitu vingine vilivyokamatwa na polisi, Dar.

“Wakitaka kujua ukweli juu ya tukio hilo wakawaulize mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, aliachwa na wenzake (ambao ni watuhumiwa) waliokuwa na bodaboda, akaambiwa kusimama akamfuata askari mwenye silaha kwa ajili ya kumpora.

“Kwa hiyo kilichofanyika ni sahihi, ukiingia kwenye laini ya uhalifu tunakugonga, Watanzania walio wengi wanataka amani, hatuwezi kuwavumilia watu wachache wanaotaka kuivuruga amani ya nchi yetu. Hatuwezi kumuua raia mwema asiye na hatia,” alisema.

Kamanda Sirro aliwatahadharisha wananchi kuhusu wizi mpya ulioibuka ambapo alisema  mtuhumiwa mmoja, Dunia Hamisi (36) mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam alikamatwa kwa madai ya kupora watembea kwa miguu kwa kutumia gari lenye usajili namba T 732 BAZ aina ya Toyota Cresta GX100.  

Alisema mtuhumiwa anayehojiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika ambapo tayari amewataja wengine anaoshirikiana nao katika uporaji huo.

VIDEO: ALICHOKIZUNGUMZA SIRRO

Leave A Reply