The House of Favourite Newspapers

SISTER FAY HEBU KUA KIDOGO BASI!

KWAKO msanii wa Bongo Fleva, Sister Fay, habari zako? Habari za siku nyingi? Bila shaka umzima wa afya na unaendelea na majukumu ya kila siku ya kuhakikisha mkono unakwenda kinywani na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa letu.

 

Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima namshukuru Mungu maisha yanakwenda kasi, mambo ni mengi muda nao ni mchache!

Nimekukumbuka kwa barua leo maana wakati mwingine kutokana na wingi wa haya majukumu siyo rahisi sana kuonana lakini kupitia barua hii, nina imani ujumbe utakufikia moja kwa moja kupitia gazeti hili au hata kwa wapambe wako.

 

Dhumuni la kukuandikia barua hii ni kutaka kukumbusha wajibu wako kama msanii, kama kweli umeingia kwenye kilinge cha sanaa kwa moyo wa dhati.

Kama kweli umeingia katika sanaa ukiwa na maengo nayo basi ubadilike, lakini kama umepotea njia basi ni vyema ukawaachia wenye malengo na sanaa wakaendelea kuliko wewe kuwapaka matope na wenzako wote waonekane wana akili kama za kwako.

 

Binafsi sikufurahishwa na picha zako za faragha zilizosambaa hivi karibuni, unaonekana umejitoa ufahamu, mambo yasiyopaswa kuonekana hadharani wewe unayaonesha bila wasiwasi. Tena unajiachia kabisa kuonesha unachokifanya kinakuvutia, umekifanya kwa moyo mweupe kabisa kwa kweli inasikitisha sana!

Kwa umri wako wewe kufanya mambo ya kipuuzi kama yale tena ukizingatia wewe ni mtoto wa kike kwa kweli inatia kinyaa. Unamuonesha nani maungo yako ya faragha tena unakatikakatika ili iweje? Unataka wanaotazama hiyo video mitandaoni wakuchukuliaje?

 

Unajiabisha Dada yangu, kama unaona muziki unakushinda ni vyema ukaacha na kutafuta shughuli nyingine. Yawezekana bahati haipo katika muziki, tafuta upande mwingine wa kusaka shilingi.

Nakumbuka uliwahi kukutana na Naibu Waziri wa Sanaa, Habari, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza, ukamtambulisha mchumba wako na kumuahidi kufanya mambo makubwa sasa huoni unajiabisha hata kwa waziri sasa hivi?

 

Ifike mahali ufanye mambo basi yanayoendana na umri wako, wewe siyo mtoto mdogo kwa nini ufanye mambo kama yale? Nakusihi sana ubadilike, muziki ni kazi kama zilivyo nyingine, kama kweli upo serious fanya, kama huwezi acha.

Usiwaharibie wenzako, kama unafikiri hizi ni kiki za kukupandisha, nikwambie tu hizi zinakushusha. Fanya kwanza kazi kiki fanya baada ya kazi nzuri. Nikiulizwa mimi hata kazi yako moja ya maana jibu nitakwambia siijui.

 

Haujanishawishi katika kazi zako, acha masihara kama kweli unataka kutusua. Bahati mbaya sana siku hizi kuna sheria ya makosa ya mitandao na mnashughulikiwa kweli wewe huoni? Basata na TRA wapo macho sasa wewe jione mjanja siku utaingia kwenye kumi na nane zao, kitakachokukuta usimlaumu MTU.

Nikutakie mabadiliko mema kama utakuwa umenielewa. Mimi ni wako katika ukusoaji wenye tija,

Anko Nangale.

BARUA NZITO | Na ANko Nangale | Maoni & Ushauri +255 718 400 146

Comments are closed.