Sister Fey Aibukia Singeli

ANAPIGA miguu yote! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Faidha Omary ‘Sister Fey’ kuanzia kwenye filamu, akaja muziki wa Bongo Fleva na sasa amehamia kwenye Singeli.

 

Akibonga na Over Ze Weekend, Sister Fey aliyejipatia umaarufu baada ya kuonekana mara kwa mara akibadilisha ‘vibenten’ alisema, ameamua kubadilika kutokana na soko la muziki linavyohitaji.

 

“Nim-ejaribu kuang-alia kwe-nye soko la muziki wa Bongo Fleva kwa sasa yupo nani wa kike, nikaona kuna Ruby, Maua Sama, Nandy na wengine ambao siwezi kufukuzana nao hivyo nimeamua kujikita huku kwenye Singeli na Vanga.

 

“Tayari nimeachia wimbo wangu wa Nimeshtuka ambao unaelezea vijana wasiopenda kufanya kazi na mambo mengi. Sister Fey huyu ni tofauti, nawaomba tu waingie kusikiliza watanipa majibu wenyewe na hapo bado hatujakutana jukwaani,” alisema Sister Fey na kumalizia kwa kicheko.

 

Katika Bongo Fleva, Sister Fey amewahi kuachia nyimbo kadhaa na kukubalika zikiwemo Wasinichapie, Kaja Mwenyewe, Chozi Langu na nyin-gine nyi-ngi.


Loading...

Toa comment