Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe leo amesema kuwa Jeshi la Polisi imewakamata watu sita kwa makosa ya kukutwa na jumla ya meno 28 ya tembo katika eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza, Prof. Maghembe amesema kuwa pembe hizo za tembo zina uzito wa zaidi ya kilo 300. Aidha imeelezwa kuwa mmoja wawaliokamatwa ni imamu wa msikiti huko Mbezi Beach.