The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (12)

0

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (12)

 

ILIPOISHIA JANA…

“Boboooooh!” ilipigwa honi. Tukaingia ndani ya gari. Nilimkuta yule dada jirani yangu amekaa kajiinamia. Nilitambua kilichomtesa. Muda wote wa safari alikuwa akichezea simu. Sasa simu ilichukuliwa na wajinga wale. Ili Kuepusha kuwa sehemu ya matatizo yake, sikumsemesha.

ENDELEA KUISOMA…

 

Safari iliendelea salama salmini na hatukukutana na tatizo jingine. Saa kumi na moja jioni tulifika mkoani Kigoma. Haikuwa mara yangu ya kwanza kuwa katika mkoa huu, niliufahamu vyema.

 

Nililala katika nyumba ya kulala wageni maeneo ya Mwanga. Kwa kuwa nilichoka sana, niliamka saa saba mchana.

 

Sikufahamu ni wapi ningempata mzee Samike. Aliyenielekeza hakunipa maelezo kamili. Mambo yakawa magumu.

 

Hata hivyo sikukata tamaa. Saa nane mchana nilitoka kwenda kumtafuta mzee nisiyemfahamu japo kwa sura tu. Nilianza msako wa barabara kwa barabara. Kila mpita njia niliyekutana naye nilimwuliza: “Unamfahamu mzee Samike? Ana nywele nyeupe, ndevu nyeupe, sharubu nyeupe, nyusi nyeupe… pia amejaa misuli.” Wote walijibu: hapana. Nikarudi katika chumba changu niliyejaa uchovu na unyonge… BOFYA  HAPA KUSOMA ZAIDI

Leave A Reply