SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (6)

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (6)

Ilipoishia jana…

Maneno ya mzee hayakuwa kichekesho, lakini yalitosha kuitwa mzaha uliolenga kuniweka sawa kiakili. Alisema maneno yale akitabasamu. Akili yangu iliyochemshwa kwa mawazo, hofu na woga, ikaanza kupoa.

 

ENDELEA KUISOMA…

 

Nilimaliza kula mhogo wangu kama ilivyokuwa kwa mzee. Babu huyu alikohoa kidogo.

 

“Haya kijana, tafadhali nieleze kinachokusumbua,” mzee aliomba akiwa kanikazia macho. Sikuwa na sababu ya kuficha maradhi, nikatengeneza sauti yangu vizuri ili nieleze mkasa wote. Lakini kabla sijafungua kinywa, mlango ukagongwa. Wote tukazigeuza shingo kuelekea ilikobishwa hodi!

 

Nilishtuka, lakini nikajikaza na kutulia mkekani. Aliyebisha hodi akaingia bila ruhusa. Mapigo ya moyo yakarudi katika kasi yake ya kawaida pale nilipomwona mtoto mdogo akijongea taratibu.

 

Mtoto alitusalimu kisha akaliinamia sikio la mzee na kuanza kunong’ona. Sikuweza kusikia alichozungumza, alikuwa fundi wa kung’ata sikio. Alipomaliza kutoa taarifa, alitoka ndani. Akairudia njia aliyotumia kuja.

 

“Haya kijana, nieleze kilichokusibu,” mzee alizungumza kwa upole na utulivu.

 

Nilimsimulia mkasa wangu wote ulionifika. niliposimulia jambo la kusisimua, alitikisa kichwa, wakati mwingine alitoa sauti za mguno kuashiria alinisikiliza.

 

“Pole sana kijana…” alisema akikunja mguu, “ni lazima ukubali kwamba ulifanya makosa makubwa kulala na mwanamke juu ya kaburi… hakikuwa kitendo cha kiungwana!”

 

“Najuta mzee wangu, ni ujinga ulinivaa,” nilijitetea.

 

“Ni bahati kama unakumbuka lilipo kaburi hilo… itarahisisha mambo aliyoyashindwa mganga wako.”

 

“Nisaidie mzee!” niliomba. Mzee akashika sharubu zake kwa maringo, akarekebisha sauti na kuendelea kuzungumza:

 

“Unaweza ukakumbuka kaburi limeandikwa jina gani?”

 

“Ndiyo,” nilijibu nikiua mbu mkubwa aliyetaka kuinyonya damu yangu mchana kweupe, “limeandikwa KIMOTA S. SAMIKE.”

 

Mzee aliposikia jina hilo alishtuka. Akanitazama usoni kwa huruma, nami nikamtazama kwa jicho lililosema, ‘nisaidie mzee wangu.’

 

“CHIMOTA S. SAMIKE!” mzee aliendelea kulitaja jina hilo, alishindwa kuficha hisia zake. Alisikitika, akanyong’onyea, macho akayatoa pima, kisha akaagiza aletewe tumbaku, bila shaka alitaka kunena maneno mazito sana juu ya CHIMOTA S. SAMIKE.

 

Wakati hayo yote yanatokea, nikaishiwa matumaini. Nikajikuta nikitamka maneno bila hiyari yangu. “Nimekwisha.”

 

Itaendelea Jumatatu…


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment