Sitogombea nafasi ya Uspika – Anne Makinda

MAKINDA

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa.

MAKINDA 2

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.

MAKINDA 3

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

(Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii)

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing’atua rasmi na kuachana na uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.

Ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.
Anne amesema kuwa “Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika”

Aidha Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.

Hata hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.

Anne amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.


Loading...

Toa comment