The House of Favourite Newspapers
gunners X

Siyo kazi rahisi Mondi kununua Ndege

0

DAR: Hivi karibuni imesambaa video ya ndege mitandaoni aina ya Airbus A 350-1000 ambapo wananzengo wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa mzigo huo ni mali ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond au Mondi’ na hivi karibuni utaingia Bongo, Ijumaa limeichimba ishu hiyo na kubaini ugumu wake.

ILIPOANZIA

Katika mtandao wa Instagram, akaunti ya mtu anayejiita Issaazam, ndiye alikuwa wa kwanza kuiposti video ya ndege hiyo na kuandika hivi:

“Asante Mungu, ile ndege aliyonunua Boss big Diamond, ndiyo inamaliziwa kuja nchini Tanzania, kaeni mkao wa (akaweka emoj za ndege) 2020 WCB4life Atukwepeki.”

MAONI KAMA YOTE

Baada ya jamaa huyo kuposti video hiyo, maoni mbalimbali yalimiminika katika posti hiyo ambapo wapo waliopongeza lakini wengine waliponda.

“Hivi anajua Airtime cost au amekurupuka? Hahahahaha kununua anaweza, lakini kuitumia itakuwa ndoto. Bado hajafikia level hizo, japo tunamuombea alafu ndege siyo kama gari, ukijisikia unanunua na barabara yoyote unaendesha tu,” aliandika Sukubeemmanuel. “Mwaka huu watajinyonga wengi sana,” aliandika Yusuphbuhuku.

IJUMAA LAFUATILIA…

Ijumaa lilifuatilia maoni ya watu wengi kwenye mitandao na kuona wengi wameamini ndege hiyo ni ya Mondi, lakini shaka yao ikawa tu ni juu ya kumudu gharama za uendeshaji.

Mbali na mitandaoni, wengi waliozungumza na Ijumaa kuombwa maoni yao, walisema hataweza kugharamia ndege kubwa kiasi hicho na kumshauri msanii huyo kujaribu kufikiria mara mbilimbili, kama anataka kumiliki ndege ni vyema angenunua ndogo.

“Lile ni dege kubwa sana, gharama zake za kuiendesha ni kubwa mno. Sidhani kama Mondi ataweza, bora angenunua ndogo,” alisema Abdu Kibando wa Sinza Dar.

DIAMOND ANASEMAJE?

Baada ya mambo kuwa mengi, Ijumaa lilimtumia ujumbe mfupi Diamond kupitia namba yake ya WhatsApp ambapo alisoma maelezo yote yaliyotaka ufafanuzi wa ndege hiyo bila kujibu chochote.

FELA AFUNGUKA

Katika kusaka ukweli wa mambo, Ijumaa liliwatafuta mameneja wa Mondi ambapo wa kwanza alikuwa ni Said Fela ambaye alipopatikana alijibu haya:

“Wewe subiri kama ndege ipo itakuja, ikishakuja ndipo tutazungumza sasa, tusubiri. Siwezi kuongea kitu ambacho hakipo,” alisema Fela.

TALE AKANUSHA

Kwa upande wake meneja wa msanii huyo, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ alipoulizwa kuhusu suala hilo, alicheka na kusema kwamba hiyo ndege siyo ya Diamond na si kazi rahisi kununua ndege.

“Si kazi rahisi kununua ndege kama watu wanavyodhani. Hivi nyie mnadhani kununua ndege mchezo? Siyo mchezo hata kidogo, hayo mambo siyo ya kweli watu wamezusha tu, Diamond hawezi kununua hiyo ndege,” alisema Tale.

ALIWAHI KUANDIKA

Suala la Mondi kuonesha dhamira ya kutaka kununua ndege si mara ya kwanza kuzungumzwa, mwaka 2014 kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mondi aliweka picha ya ndege na gari kisha kusindikiza na ujumbe ulioashiria kuwa na ndoto ya kumiliki ndege. “Tuseme ishaaallah#2014 JustWaitAndSee kwani wao wamewezaje hadi we ushindwe WCB for live darling,” aliandika Mondi.

ALITAMBA NA MABASI

Hivi karibuni tetesi zilivuma tena kwamba msanii huyo yupo mbioni kununua mabasi ambayo yatakuwa yanabeba abiria kwenda mikoani, ambapo meneja wake Tale alikiri kuwepo kwa mabasi hayo na kusema kwamba watu wawe wavumilivu kwani muda si mrefu magari hayo yataanza kufanya kazi, lakini hadi sasa bado mabasi hayo hayajaonekana mjini.

 

Stori: MEMORISE RICHARD NA NEEMA ADRIAN, Ijumaa

Leave A Reply