#GlobalCelebrityUpdates: Skales Asimulia Jinsi Alivyolazimika Kumkana Mama Yake Zaidi Ya Mara Moja.

Kwenye celebrity updates za leo machi 8 2017, nakusogezea hii ya staa wa muziki kutoka Nigeria Skales.

Hit maker wa single ya ‘Shake Body’ Skales hivi karibuni alifanya interview na kpindi cha Radio kiitwacho ‘Saturday Beats’ huko Nigeria na kuongea vitu vingi ikiwemo tabu alizozipata kabla hajawa staa na kusema alishawahi kulazimika zaidi ya mara moja kumkana mama yake mzazi.

 Baba yangu alitutelekeza nikiwa mdogo sana, hata sijui anafananaje… Mimi na mama yangu tulilazimika kulala kwenye frame za baishara kipindi hicho nipo shule ya msingi hali iliyoendelea mpaka nilivyofika secondari. Kitu pekee kilichokuwa kinanipa matumaini ni muziki… ” – Skales

Aliendelea kusumilia:

Ilifika hatua nikafukuzwa shule kwasababu nilikuwa siwezi kulipa ada ya shule. Nilikuwa pia nalazimika kuiba sare za shule kwasababu zangu zilikuwa zimechakaa kupita kiasi na mama akiniuliza namwambia tu nimeweka hela mpaka ilipotoshea kununua sare mpya…

Badaae mama yangu aliazna kufanya kazi ndogondogo na za udobi kwenye nyumba za marafiki zangu kitendo kilichoniumiza sana, nakumbuka nililazimika kumkana mama yangu mara nyingi kutokana na kuona aibu ya maisha yetu, pia sikuwahi kuwaruhusu marafiki zangu wajue naishi wapi maana wengi wao walikuwa watoto wa vigogo.

Nilipo mwambia mama kuwa nahamia Lagos aliniomba nimalize elimu yangu ya chuo kikuu lakini nilimshawishi kuwa maisha ya kule nitayaweza akakubali…” – Skales.

 Hayo kwa sasa ni historia kwa msanii huyo ambaye hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha ya nyumba aliyomjegengea mama yake na kuandika caption fupi ya kutia moyo. Icheki picha hiyo hapa chini.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.


Loading...

Toa comment