The House of Favourite Newspapers

SMART CODES YABORESHA MWONEKANO WA NEMBO YAKE

Meneja Mkuu wa Kampuni   ya Smart Codes inayojishughulisha na utoaji wa huduma za Kiteknolojia na matangazo, Bruce Magaisi (kushoto) na Mkurugenzi wa  Mtendaji wa Kampuni   hiyo, Edwin Bruno  (kulia) wakimsikiliza Meneja wa Smart Lab, Juliana Kayombo, (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  kuhusiana na program anayolenga kuinua vipaji vya wanafunzi  wa vyuo vikuu nchini  inayoendeshwa na Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni   ya Smart Codes inayojishughulisha na utoaji wa huduma za Kiteknolojia na matangazo, Edwin Bruno (wapili kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  wakati wa hafla ya  kutangaza uboreshaji  wa mwonekano  wa nembo yake mpya  na utoaji wa huduma zake na program mbalimbali   hususani ya  vyuo vikuu. Kutoka Kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo , Bruce Magaisi,  Meneja wa Smart Lab, Juliana Kayombo  na  Mkuu wa Miradi na bidhaa  Ruben  Mussa.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Smart Codes inayojishughulisha na utoaji wa huduma za Kiteknolojia na matangazo, wakimshuhudia Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni   hiyo, Edwin Bruno  (katikati) akibofya kitufe cha kompyuta  wakati wa hafla ya    kutangaza uboreshaji  wa mwonekano  wa nembo  yake mpya  na utoaji wa huduma zake na program mbalimbali   hususani ya  vyuo vikuu.

 

 

KAMA moja ya maendeleo, Kampuni ya Smart Codes inayohusika na utoaji wa huduma za kiteknolojia na matangazo jijini Dar es Salaam, imeboresha mwonekano wake ikiwa ni pamoja na bidhaa na huduma zinazotolewa ili kukidhi mahitaji ya wateja wake kuendana na mabadiliko na maendeleo ya kibiashara.

 

 

Smart Codes imeboresha muonekano wa nembo yake ya mbuni na kuifanya iwe na mvuto zaidi kama kiashiria cha hatua kubwa ya mabadiliko na kimaendeleo iliyopiga kampuni hiyo ukilinganisha na hapo awali. Mabadiliko hayo yamekuja sambamba na maboresho ya ufanyaji kazi, ikilenga zaidi umakini na ufanisi unaoendana na dunia ya leo inayoendeshwa kidigitali na kiteknolojia.

 

 

“Maboresho haya yalianza mwanzoni mwa mwaka huu tulipoamua kuboresha mfumo wa jinsi tunavyofanya kazi zetu. Tumeamua kwanza kuanza na mabadiliko ya ndani ya kampuni, kisha kufanya maboresho mengine. Lakini la muhimu limekua ni kuboresha mwenendo wetu kiofisi, jinsi tunavyofanya kazi, ikiwa ni pamoja na utaratibu tunaotumia katika kuajiri wafanyakazi wabunifu na mazingira yetu ya ufanyaji kazi kiujumla” Alisema Edwin Bruno mkurugenzi wa kampuni ya Smart Codes wakati akiongea na waandishi wa habari. “Pia tumechukua muda kuchanganua mifumo ya kibiashara kwa wateja wetu tukizingatia hali ya kisayansi na teknolojia. Tumegundua kwamba makampuni mengi yanahitaji mikakati na mifumo imara ya kuendesha biashara kiteknolojia zaidi. Na Smart Codes tumejikita katika kusaidia makampuni hayo” aliongeza Edwin Bruno.

 

 

Kati ya huduma 16 zinazotolewa na Smart Codes kulingana na kanuni zake za utoaji huduma ni pamoja na kutengeneza mikakati ya kibunifu, kutengeneza maudhui ya mawasiliano ya kidijitali, kujenga mahusiano ya kibiashara kwa njia ya mitandao, kutengeneza muonekano unaokubalika kijamii kwa bidhaa, huduma na makampuni, kununua nafasi za matangazo, kuleta suluhu bunifu za kibiashara, kutengeneza mifumo ya kuendesha mashindano ya bahati nasibu, kufanya utafiti kidijitali, kutengeneza tovuti zenye kiwango pamoja na kutengeneza aplikesheni za simu.

 

Kulingana na huduma hizo zinazotolewa, Smart Codes wana wateja wa aina mbalimbali kulingana na mahitaji yao. Kuna wateja wanaohitaji mikakati ya kuboresha biashara zao au kuingiza bidhaa mpya au huduma mpya sokoni.

 

“Kwa sasa tuna studio ya video, picha, sauti na grafiks inayoweza kuwasaidia wateja wetu kutengeneza matangazo ya televisheni na ya redio kwa ubora wa hali ya juu na kwa ubunifu mkubwa” alisema Edwin Bruno.

 

Alimalizia kwa kutambulisha kitengo kipya, akisema, “Smart Lab ni kitengo ndani ya Smart Codes, na lengo kubwa ni kuwawezesha wanafunzi wa elimu ya juu wenye mawazo ya kibiashara waweze kusimama wenyewe na kujitegemea kama kampuni wanapohitimu”. Aliendelea kusema, “Smart lab itawapa usaidizi wa kitaalamu na kuwahamasisha ili kuhakikisha wanakua kibiashara kwa kuwaleta karibu na makampuni yanayohitaji huduma au suluhu bunifu za kibiashara kwa kuwajengea mahusiano endelevu.

Kwa mawasiliano ya ziada:

Smart Codes [email protected]

Simu: +255 222 775 801

 

Comments are closed.