The House of Favourite Newspapers

Snura Afunguka Skendo ya Kukwapua Bwana!

 

Snura Mushi.

MSANII wa filamu Bongo, Snura Mushi amefungukia uvumi wa kumkwapua bwana aliyekuwa anatoka na msanii mwenzake, Salma Jabu Nisha aitwaye Minu na kusema kuwa, jamaa
huyo ni mtu wake wa karibu tu siyo kimapenzi.

    Salma Jabu Nisha

Balaa hilo liliibuka siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii baada ya msanii huyo kumtakia heri ya kuzaliwa Minu kwa maneno matamu ambayo watu walianza kujaji kuwa huenda ni wapenzi, ambapo alifunguka kuwa hana uhusiano na mwanaume huyo kwani ukaribu wao ni wa kikazi si zaidi.

 

“Huyo Minu siyo mpenzi wangu na wala sina muda mrefu tangu nijuane naye, kuna siku alinitafuta baada ya kupewa namba yangu na Nisha, sababu alikuwa ameandika wimbo ambao aliona nafaa kuuimba, sasa kumtakia heri ya kuzaliwa kwa kumwambia nampenda ndiyo kosa?”alihoji msanii huyo.

Stori: Mayasa Mariwata

Comments are closed.