The House of Favourite Newspapers

Snura, Mashauzi, R.O.M.A ndani ya Dar Live

0

romaR.O.M.A Mkatoliki.

MASTAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura na R.O.M.A Mkatoliki, wakali wa Singeli, Man Fongo na Shoro Mwamba wanatarajiwa kuungana na wakali wa Taarab, Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi, Juni 4, mwaka huu na kugonga shoo ya kihistoria ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

snuraSnura Mushi.

Akizungumza na Over Ze Weekend Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa shoo hiyo itatambulika kama Usiku wa Nani Mkali ambapo mpango mzima utaanzia saa mbili za usiku. Snura na R.O.M.A Mbizo alisema kuwa usiku huo kwa upande wa Bongo Fleva, burudani itawashwa na Snura na R.O.M.A ambao watapiga nyimbo zao zote kali.

isha pichaIsha Mashauzi.

“Mashabiki watarajie kusikia ngoma kibao kutoka kwa Snura kama vile Nimevurugwa na Majanga.
“Pia R.O.M.A ambaye ni mkali kunako Bongo Fleva, atalishambulia jukwaa kwa kupiga ngoma zake zote kali kuanzia Mathematics, 2030, Mtoto wa Kigogo na nyingine nyingi.”

Mashauzi Classic Kwa upande wa Muziki wa Taarab, Mbizo alisema kuwa Kundi la Mashauzi Classic likiongozwa na Isha Mashauzi litatoa burudani mwanzo mwisho. “Mashauzi Classic itafunika na nyimbo zao zote kali kuanzia Mapenzi Hayana Dhamana, Mapenzi Yamenivuruga, Nimpe Nani na nyingine nyingi,” alisema Mbizo.

Man Fongo na Shoro Mwamba Wakali wanaokimbiza kunako Muziki wa Singeli nao watakuwepo kulishambulia jukwaa ambapo nao watakimbiza ‘mperampera’ na ngoma zao zote ambazo ni habari ya uswahilini kwa sasa.

“Singeli itahamia Dar Live kwa mara nyingine, Man Fongo anayebamba na ngoma kali kama Hauna na Hainaga Ushemeji usiku huo ataimba na kucheza na mashabiki ngoma zake hizo huku naye Shoro Mwamba akihamshahamsha na ngoma ya Sembe Tembele,” alimaliza Mbizo.
Burudani hiyo itakayokwenda kwa kiingilio cha 8,000 tu getini, imedhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money Tap Tap.

Leave A Reply