The House of Favourite Newspapers

Snura: Mume Si Kitu cha Mchezomchezo Nyie Mume

Snura Mushi

MWANAMUZIKI Snura Mushi ameibuka na kusema kuwa, si kwamba hataki ndoa, anaitaka sana lakini akatahadharisha kuwa, mume si kitu cha mchezomchezo hivyo ni vyema kujipanga na kutokurupuka.

 

Snura alifunguka hayo baada ya kuulizwa kwamba endapo leo atatokea mwanaume na akataka kumuoa, atakuwa tayari? Jibu lake lilikuwa hivi:

 

“Kiukweli siwezi kukubali kirahisi hivyo eti kwa sababu tu nimetajiwa ndoa, ni lazima nimjue kwanza mtu ni wa aina gani kwani hayo ni maisha yangu.

 

“Nikiingia kichwakichwa, mwisho wa siku nitaumia na nitakuwa na historia nyingine kabisa kwani sitavumilia,” alisema Snura. Akaongeza kuwa, siyo kwamba yuko singo, mpenzi anaye ila hilo la ndoa ndilo ambalo inabidi kujifikiria sana kabla ya kulipa nafasi ili kuepuka kuja kujuta baadaye.

STORI: HAMIDA HASSAN

Comments are closed.