The House of Favourite Newspapers

Snura Naye Kuiburuza Kampuni Mahakamani

0
Mwanamuziki Snura Mushi.

WAKATI marapa marafiki Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wakiwa wamekaa mkao wa kula kusubiri mamilioni ya shilingi walizoshinda mahakamani kama fidia kwa kampuni moja kutumia wimbo wao bila idhini, Snura Mushi ambaye ni mkali wa Bongo Fleva, naye anatarajia kuiburuza mahakamani kampuni moja ya unga kwa kutumia wimbo wake wa Majanga kwenye matangazo yao bila makubaliano.

 

Akibonga na Za Motomoto News, Snura alisema tayari mwanasheria wake amewapelekea ‘notice’ ya siku saba akiwataka kumlipa fidia ya shilingi bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake hivyo kama hawatajibu chochote kesi hiyo itapelekwa mahakamani.

 

“Kiukweli nimesumbuka kwa muda mrefu sana tangu mwaka 2015, nimewahi kuwatafuta wanasheria watatu ikashindikana, nikaenda COSOTA nako hakuna kilichoeleweka lakini kwa sasa nimepata mwanasheria mwingine ambaye naamini atafanikisha na nitapata haki yangu maana ushahidi na kila kitu kipo,” alisema Snura.

STORI: GLADNESS MALLYA

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply