The House of Favourite Newspapers

Snura, Ney, Stamina, Mc Kinata, Chegge Chigunda, Maua Sama Waiteka Tmk kwa Tamasha la Zege Day

0
Mashabiki wa muziki wakiangalia Tamasha la Zege Day

WASANII mbalimbali Leo wamefanikiwa kuusimamisha ukanda wa Wilaya ya Temeke na viunga vya jirani Jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha mashabiki mbalimbali kwenye tamanasha la Kimataifa lililofahamika kama ‘Zege Day’ lililofanyika kwenye viwanja vya Mwenbe Yanga

 

Tamasha Hilo ambalo lilinogeshwa na wasanii wenye mvuto katika miondoko mbalimbali ikiwemo singeli, bongofleva na muziki wa dansi ni pamoja na Ney wa Mitego, MC Kinata, Maua Sama, Snura Mushi na Mwanamuziki  mkongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi Josse Mara.

Stamina naye alikuwa sehemu ya wasanii waliokiwasha katika Tamasha hilo la Zege Day

Mbali ya wasanii hao wengine walio amsha hisia pindi walipopanda jukwaani ni pamoja na msanii Stamina.

 

Huku wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo la ‘Zege Day’ ni  pamoja na Dayoo,Micky Singer,Rasco Sambo,Lody Music, Sir Jay, Nedy Music, Kayumba, Mzee wa Bwax na Sholomwamba

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati Tamasha Hilo likiendelea mmoja wa viongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group (MMG) Sebastian Maganga alilielezea Tamasha Hilo la Zege Day kwa kusema

Tamasha la Zege Day lengo lake kuu ni kutoa fursa ya ajira kwa vijana

kuwa ni la Kimataifa na linafanyika  duniani kote  hivyo wao MMG wameratibu ikiwa ni katika kutambua na kuthamini mchango wa vijana wauza Chips kwa kuwarahisishia wakaazi katika maeneo mbalimbali kupata chakula cha haraka.

 

” Sote tunajua kuwa  maisha ya kimjini yanaratiba ndefu na pana na hapo ndipo utamaduni wa Zege ulipoanzia  sisi kama Clouds tumejikita katika kutoa ajira  kwa vijana  ndipo tulipokaa na kukubaliana kuja kufanya Tamasha hili hapa Mwembe Yanga baada ya wapenda Zege lialia kupiga kura” alisema Maganga.

Burudani ya muziki ilikuwa ni sehemu ya kunogesha Tamasha la Zege Day

Maganga aliongeza kwa kusema kuwa hakuna historia kamili wapi ilikoanzia Chips Zege lakini historia inasema kuwa watanzania wenye asili ya Bara la Asia ndiyo walianza kuuza Chip’s maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam na baadaye chakula hicho kikajizolea umaarufu.

Msanii Snura akiwa Stejini

Aidha Maganga amewashukuru wadhamini wa Tamasha Hilo ambao ni kinywaji baridi cha Pepsi,The Kick na wazalishaji wa sausages.

Leave A Reply