The House of Favourite Newspapers

MAISHA YA SOLO THANG ‘TRAVELLAH’ UGHAIBUNI

Tokeo la picha la SOLO THANG
Solo Thang ‘Travellah’ na Mwanae

MWISHONI mwa miaka ya 1990, Clouds Media ikishirikiana na Kinywaji cha Pilsner, waliandaa mashindano ya kusaka vipaji vya wanamuziki yaliyofanyikia kwenye Ukumbi wa Mambo Club.

 

Vijana wengi walijitokeza kutoka viunga mbalimbali vya Jiji la Dar, na majaji kwenye mashindano hayo walikuwa ni maprodyuza maarufu, P Funk Majani, Dunga na Master J.

 

Mashindano yalikuwa na msisimko mkubwa na washindi waliopatikana kwenye mashindano hayo walikuwa ni vijana wanne kutoka Kijitonyama waliounda kundi liitwalo Cewer Cellibacy, ambao ni Jay Moe, Jaffarai, Mchizi Mox na Kelvin Kimali kwenye upande wa muziki wa kughani na mshindi wa pili alikuwa ni mshikaji kutoka Mbagala, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.

 

Washindi hawa na washindi wa upande wa Muziki wa Rege, ambao mshindi wa kwanza alikuwa ni Mack 2B (marehemu) na mshindi wa pili Lady Lou (marehemu) waliungana na kuunda kundi la Wateule.

Akiwa Wateule, Solo Thang ndiko alikofahamikia zaidi lakini kama mwanamuziki, solo amefanya albamu nne ambazo ni Homa ya Dunia, Kina cha Chini, Kilio Changu na I’M Travellah. Baadhi ya nyimbo zilizofanya afahamike zaidi ni pamoja na Mambo ya Pwani, Tafadhali, Nakuwaza, Miss Tanzania na Kina cha Chini.

 

Kwa muda sasa Solo Thang hayupo Bongo. Makazi yake pamoja na familia yake ni Uingereza na Mikito Nusunusu imefanya naye mazungumzo dairekti na amefunguka kuhusu muziki na mambo yake binafsi. Huyu hapa;Tokeo la picha la SOLO THANG

Mikito: Muziki vipi kwa sasa, mbona upo kimya?

Solo Thang: Ni kweli nipo kimya. Sababu ni kwamba hapo nyuma kidogo nilikuwa bize na masomo. Nilikuwa chuo nasomea masuala ya biashara. Kuhusu muziki mpaka kufikia mwezi Desemba nitaanza kuachia kazi kwani kwa sasa ninachofanya naandaa projekti kadhaa ili nichague ipi ianze na ipi ifuate.

Mikito: Wewe ni mwanamuziki mkongwe, unazungumziaje Muziki wa Hip Hop ulipofikia kwa sasa Bongo?

Mikito: Muziki wa Bongo huko ulipo una impakti gani?

Solo Thang: Kiukweli mapokeo ni mazuri. Mapinduzi waliyofanya kina Alikiba, Diamond, A.Y na wengine wengi yameuweka muziki wetu kwenye

Thang: Muziki kiukweli umebadilika. Kuna ushindani mkubwa, mwanamuziki unatakiwa kuangalia soko, ‘production wise’ masuala ya video ndiyo yanamata zaidi. Kwa upande wangu nina uwezo wa kubadilika na kwenda nao sawa ingawa kuna mambo siwezi kufanya, kama ili uwe juu utengeneze kiki, uvae vinguo vya kubana na mambo mengine.Tokeo la picha la SOLO THANG

Mikito: Bongo unamsikiliza mwanamuziki gani zaidi?

Solo Thang: Nasikiliza wanamuziki wengi. Namsikiliza Alikiba, wanamuziki wa Wasafi, Fid Q, A.Y, Dogo Janja nasikiliza mpaka muziki wa kina Maua Sama na Lina.

Mikito: Mara ya mwisho kufanya shoo Bongo ni lini?

Solo Thang: Mara ya mwisho ni mwaka 2014. Niliporudi Bongo nilikutana na Wateule tukafanya mambo na nikapata nafasi ya kupiga shoo.

Mikito: Muziki wa Bongo huko ulipo una impakti gani?

Solo Thang: Kiukweli mapokeo ni mazuri. Mapinduzi waliyofanya kina Alikiba, Diamond, A.Y na wengine wengi yameuweka muziki wetu kwenye ramani. Si jambo la ajabu kukutana na Wanaijeria, Waghana, Wazungu wenyewe wakiimba muziki wetu. Klabu unapigwa sana, ingawa huwezi kuusikia mara kwa mara kwenye redio na kuona kwenye televisheni lakini kuna chaneli za Afrika tupo huku tunaona kinachoendelea.

Mikito: Unafikiri nini kinapelekea waasisi wengi kuanza kutoweka kwenye gemu?

Solo Thang: Nafikiri hilo ni suala la asili. Muda unabadilika, watu wanakua na majukumu yanaongezeka. Tegemea watu wengi wataondoka kwa sababu waasisi hawawezi kuwepo milele. Hata hawa unaowaona leo kina Bill Nas, Diamond wataondoka pia. Ipo hivyo hata kwenye maisha ya kawaida.

Mikito: Nini unapanga kufanya kama ‘legacy’ yako kwenye muziki?

Solo Thang: Nategemea kuja kufungua Bongo Studio kubwa ambayo itawasaidia wanamuziki wengi chipukizi ambao hawana uwezo wa kurekodi na pia kutakuwa na lebo hapohapo. Nitajitahidi kuwa na vifaa vya kisasa na mipango ya kisasa.

Mikito: Una mpango wa kuishi Bongo?

Solo Thang: Ni nyumbani, huwa ninarudi mara kwa mara kwa hiyo lolote linaweza kutokea.

Mikito: Mbali na muziki unashughuli gani nyingine huko unafanya?

Solo Thang: Kuna kampuni fulani ninapiga kazi kama mhasibu.

Mikito: Kuna kipindi ulikuwa unamsaidia Chid Benz, kwenye suala zima la dawa za kulevya, uliishia wapi?

Solo Thang: Kwanza niseme wazi kwamba Chid ni kama mdogo wangu, nimefanya mambo mengi na kaka yake. Niliporudi Bongo na kuzungumza naye, tulipanga namna ya kumsaidia lakini ni jambo la kusikitisha kuona mambo hayaendi vizuri. Lakini kikubwa wa kumsaidia Chid Benz wa kwanza kabisa ni yeye mwenyewe na si mtu mwingine.

Mikito: Naona unapromoti sana brandi yako ya mavazi mtandaoni, I’M Travellah, unaweza kuizungumzia.

Solo Thang: Yah! I’M Travellah ni brandi ya mavazi ambayo nimeifanya kwa kulenga zaidi wasafiri. Wanaokwenda sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutafuta maisha na hata wafanyabiashara. Lakini pia, hata watu wote duniani tunasafiri, haya si makazi yetu, kwa hiyo ni brandi ya kila mtu na tumepanga makubwa kwa ajili ya baadaye.

Mikito: Vipi kuhusu familia?

Solo Thang: Nina watoto wanne ninaoishi nao huku. Kuna Yassir mwenye miaka 11, Zainab miaka 9, Zain ana miezi nane, Bongo nina mtoto mmoja ana miaka 14 anaitwa Faris, mke wangu ni Mbongo, ndiye nimezaa naye watoto ninaoishi naye huku.

Comments are closed.