The House of Favourite Newspapers

Solskjaer: Msimponde Ronaldo Mtaumbuka

0

KOCHA wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kama kuna mtu anataka kumponda Cristiano Ronaldo basi aangalie mechi kati ya Man United na Atalanta.

 

Ronaldo juzi alifanikiwa kuibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake ya Man United bao la ushindi kwenye matokeo mazuri ya 3-2 waliyoyapata katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

“Kama kuna mtu anataka kumponda Ronaldo anatakiwa kuangalia kiwango chake kwenye mchezo huu.

 

“Anatakiwa kuona jinsi ambavyo amekuwa akijituma uwanjani, amtazame jinsi ambavyo amekuwa akikimbia, ni mchezaji mzuri sana mbele ya lango, bao alilofunga ndiyo linaonyesha ubora alionao,” alisema kocha huyo.

Leave A Reply