testiingg
The House of Favourite Newspapers

SPC Yakabidhi Rasmi Viwanja kwa Washindi Kili Marathon

0
Meneja Masoko wa SPC, Catherine Michael akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

Septemba 30, 2022: Kampuni ya Surveyed Plots Company Ltd ya Jijini Dar es Salaam leo imekabidhi rasmi zawadi ya viwanja kwa wanariadha wawili walioshiriki mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022 na kuibuka watanzania wa kwanza.

Angelina Yumba kushoto aliyekaa na Alloyce Simu kulia aliyekaa wakiwa wamekaa na  Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine wa heshima na uongozi wa Kampuni ya SPC kwenye hafla hiyo.                                                                                                                                                                                                                           

 

Viwanja hivyo, vilivyopo Kigamboni vimekabidhiwa kwa Alloyce Simbu aliyeshinda mbio za KM 42 kwa upande wa wanaume na Angelina Yumba aliyekuwa wa tatu katika mbio za KM 42 na mtanzania wa kwanza wa kike.

 

Wanariadha hao walikabidhiwa hati rasmi ya umiliki wa viwanja hivyo katika hafla maalumu iliyofanyika katika ofisi za SPC Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa riadha ikiwemo Chama Cha Riadha Tanzania, waandaaji wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon na wadhamini.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi, Meneja Masoko wa SPC, Catherine Michael alisema wanayo furaha hatimaye kukamilisha utaratibu wa kukabidhi rasmi viwanja hivyo ikiwemo kila mmoja kupokea hati ya umiliki.

 

“Viwanja hivi viko Kigamboni na kila kimoja kina ukubwa wa sq mita 400 na thamani ya Tsh 4,000,000 kila kimoja kama tulivyotangaza wakati wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kule Moshi mapema mwaka huu,” alisema.

 

Aliwapongeza washindi hao na kusema kampuni hiyo itaendelea kutoa zawadi za aina hiyo ili kutoa motisha na hamasa kwa wanariadha wa kitanzania kufanya vizuri zaidi katika mbio za KM 42.

 

“Tunatoa wito kwa wanariadha wengine waendelee kujifua na kujiandaa na mbio za mwakani ili nao washinde viwanja ambavyo vitaboresha maisha yao.

 

Akizungumza baada ya kupokea hati ya umiliki, Simbu alisema zawadi hiyo ni fahari kubwa kwake kwani inampa motisha ya kujiandaa vizuri zaidi kwa mbio za mwakani ili aweze kutetea nafasi yake na kushinda kiwanja kingine.

 

“Zawadi hizi ni za kweli na kama mnavyoona nimekabidhiwa cheti changu cha umiliki sasa nina kiwanja Kigamboni. Naishukuru sana SPC na waandaaji wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa kuja na utaratibu huu kwa kweli ni nhamasa kubwa sana kwetu sisi wanariadha wa kitanzania,” alisema Simbu.

 

Naye Angelina Yumba alisema hakuwahi kuwaza kumiliki kiwanja Kigamboni lakini riadha imempa nafasi hiyo ya kipekee. “Kwa kweli nina furaha sana na natoa shukrani za dhati kwa SPC kwa kutukumbuka na kuja na utaratibu huu wa kutuzawadia viwanja. Ni ubunifu wa kipekee kwa sababu hii ni zawadi ya kudumu na imeongeza thamani katika maisha yangu,” alisema.

 

SPC ni moja ya makampuni yanayoongoza katika uuzaji na upimaji wa viwanja nchini na ni moja ya wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo hufanyika kila mwaka Mjini Moshi.

Leave A Reply